INSHALLAH-INSHALLAH- INSHALLAH
Sura ya "1"
Bi Tamaa alikuwa ni mwanamke mwenye watoto wanne, watatu walikuwa ni wa kiume na mmoja alikuwa wa kike.
Bi Tamaa aliondoka kwao Shinyanga baada ya kumaliza masomo ya darasa la saba. Sababu iliyo mfanya andoke kwao hakuna aliyeifahamu. Hiyo ilikuwa ni siri yake mwenyewe.
Baba mzazi wa Bi.Tamaa, mara nyingi alipenda kunitembelea na mimi pia nikajenga tabia ya kumtembelea. Tulijenga undugu wa hiari. Mimi mwenyewe mzee huyo nikawa namwita baba.
Mzee huyo tulizoea kumwita jina Mzee wa Busara na mara nyingine tulilifiupisha na kulitamka Mzee Busa. Alijaliwa kuwa na watoto, wawili wa kiume na wawili wa kike.
Mtoto wake wa kwanza alizoeleka kuitwa Ustadhi, kwani alikuwa anapenda kuvaa kanzu anapokuwa nyumbani. Mtoto wa pili ndiyo huyo Tamaa, mtoto wa tatu aliitwa jina Adul na mtoto wa mwisho Kulthumu.
Ilikuwa ni siku ya Ijumaa baada ya ibada Mzee Busa aliniomba tubaki pale msikitini tuweze kuongea mawili matatu. Pamoja nilikuwa na udhuru, nilishindwa kumkatalia kutokana na jinsi nilivyo kuwa nina mheshimu. Siku zote, usikatae wito bali kataa neno.
Tulitoka nje ya Msikiti, tukajitenga chini ya kivuli cha mti uliokuwa maeneo yale. Ndipo aliponiambia kwa sauti ya unyoge kidogo. Nadhai umri nao ulikuwa umemkimbia, kwani alikuwa tayari ni mstaafu, aliniambia:-
"Mwanangu, nafikiri unamkubuka dada yako, ambaye alikuwa anakuja ofisini kipindi bado nipo kazini.?"
Haraka niliitisha kumbukumbu zangu, lakini wakati huo macho ya ngu yalikuwa mbali kidogo, wapita njia nao walinifanya niwe mzubaafu, unajua tena mambo ya mjini. Nilimwitikia kuwa namkumbuka, nilimtajia jina lake. Akanishika bega akaniambia:-
" Ee-waa-laa, huyo ni dada huyo, nasikia yuko mkoa wa Mwanza ama Kigoma. Sasa nakuomba mwanangu. Katika safari zako, uwe unanusa nusa. Ukimpata mwambie arudi nyumbani ni hilo tu mwanangu. Sasa twende zetu Nyumbani."
Ni kweli yule binti, namaanisha Tamaa, nilimkumbuka, ila muda mrefu uliisha pita, yaani ni miaka zaidi ya kumi na ushee hivi. Niliwaza iwapo nitaweza kumkumbuka. Kwa vyovyote atakuwa na mabaliko fulani.
Mungu si Athuman, nilipata safari ya kutembelea mkoa wa Kigoma, Mara na Mwanza. Mkoani Mwanza nilikaa takribani wiki moja. Siku hiyo nilikuwa nimekwenda Igoma kumtembelea jamaa yangu.
Huwezi kuamini, kwa mbele yangu nilipo kuwa nimesimama, nasubiri usafiri wa kurudi mjini nilikofikia. Bila mategemeo nilimuona mwanamke, wakati huo alikuwa ni mama mtu mzima, anaelekea nilipo kuwa nimesimama.
Aliponifikia, aliniita kwa jina langu huku akitabasamu. Pia mimi nilitabasamu na tulisalimiana. Tulizungumza mawili matatu, ndipo Bi Tamaa aliniomba tufuatane naye nikapafahamu anapoishi. Kwa upande mwingine ilikuwa ni bahati sana kwangu kutokana na maagizo ya Mzee Busa.
Nilifuatana naye hadi alipokuwa anaishi, palikuwa ni jirani kutoka barabara kuu. Tuliongea hili na lile kwa furaha tele. Aliniuliza habari za pale nyumbani na mimi nilikuwa namjibu kwa ufupi ufupi tu; kama vile ni nzuri, hawajambo, wapo vizuri nakadhalika.
Maongezi yetu yalitufikisha kunako saa mbili usiku. Wakati huo tayari alikuwa ameniandalia chakula, baada ya kuwa nimeisha kula nimeshiba. Nilitoa shukrani kwa ukarimu wake alionitendea, hivyo basi nilmuomba ruhusa ili niondoke nirudi mjini.
Bi. Tamaa alinikatalia kata kata kwamba haiwezekani nifike na kuondoka. Kwani bado ana mengi ya kuongea na mimi, tena imekuwa bahati sana kukutana naye, kwa vyovyote nitampa ufumbuzi wa jambo lake kwa namna moja au nyingine.
Sikuwa na namna ya kukataa, lakini nilipata wasiwasi kidogo. Nilijiuliza, muda nilio kuwa pale mbona sioni iwapo kuna baba mwenye mji? Bali nilikuta vijana wa kiume watatu na msichana mmoja. Ilibidi nimuulize:-
"Vipi shemeji yangu, huwa anachelewa kurudi?"
Ucheshi aliokuwa nao, nilimuona umetoweka ghafla. Machozi yalimjaa machoni mwake. Moja kwa moja ishara hiyo ilinipa mshituko kwamba lazima kulikuwa na tukio kubwa lililowahi kutokea. Sikutaka kudadisi, ilinilazimu nikae kimya. Bahati nzuri wale vijana walikuwa vyumbani mwao, sebuleni tulikuwa wawili tu. Bi. Tamaa alifuta mchozi yake kisha alinijibu kwa sauti ya huzuni:-
"Kaka, ndiyo maana nimekukatilia usiondoke, wewe utakuwa ni mmoja wa kutatua janga langu."
Ukweli ilibidi nitumie hekima kubwa, kumtuliza, pia kuendana naye kadri alivyotaka yeye pale palipo kuwa na ulazima. Muda nao ulikuwa unadai mapumziko. Nilimuomba nipumzike, mengine tutaongea kesho yake kwa kudra ya Mola. Alinipeleka chumba alichokuwa ameniandalia, aliniacha nipumzike.
Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Jumapili. Sikuona sababu ya kuondoka mapema kwa kuwa ilikuwa ni siku ya mapumziko. Wakati nikiwa bado chumbani, nilisikia kauli iliyonishitua kidogo. Wale vijana walikuwa wanahimizana waende Kanisani ili wawahi misa ya kwanza. Bi. Tamaa nae aliwaambia kwamba yeye hataweza kwenda akaniacha mimi mgeni peke yangu.
Niliwaza, Mzee Busa ni muumini wa Imani ya Kiislamu pamoja na familia nzima. Mbona tena huyuuuu? Jibu sikulipata palepale, nilidhalau, kwani yote ni maisha. Niliamka nikakuta nimeandaliwa maji ya kuoga bafuni, na baadae nilipatiwa kifungua kinywa.
Nilimjulisha kuwa, mimi nitakuwepo hapo kwake kwa Jumapili yote nzima. Jumatatu nitaondoka kuanza safari ya kurudi Shinyangà. Hivyo basi ni muda tosha tuutumie kuongea yaliyo muhimu.
Katika mazungumzo yetu nilikimbilia kutaka kujua wale vijana ni wana familia ipi? Alinijibu bila kuwa na ile hali aliyo kuwa nayo jana yeke, aliniambia:-
"Kaka, tusiende mbali sana. Hao vijana ni wapwa zako."
Sikuamini machoni mwangu, wale vijana walivyokuwa na kimo kimoja, rangi ya ngozi zao ni moja na walikuwa wamefanana kwa kila hali. Ilibidi nimuulize:-
"Eti unasemaje? Mbona kimo chao na kila kitu wako sawa?"
Bi.Tamaa, alicheka sana, tena sana kiwango cha kububujika machozi. Nilihisi huenda ni mchanganyiko wa furaha na majonzi, ndio maana amekuwa na kicheko cha machozi. Hata hivyo baada ya kicheko aliniambia:-
"Kaka, hao ni mapacha. Nilijifungua kwa wakati mmoja."
Mara wale vijana wakawa wamefika kutoka Kanisani. Kila mmoja alinipigia goti na kunisalimia kwa kutaja jina la 'Mjomba'. Nadhani mama yao aliisha waambia kuwa mimi ni nani kwao. Mama yao aliwaambia kwanza wabaki hapo tulipo. Hapo ndipo alianza kunitambulisha mmoja baada ya mwingine:-
"Kaka, huyu ni Kibonge ndio wa kwanza. Wa pili ni huyu hapa 'Love', mwingine wa tatu ni huyu hapa 'Kahindi'. Mwisho ni huyu 'Kitinda.' Wote nimewazaa siku moja wamezidiana dakika."
Baada ya hapo aliwaruhusu waendelee na mambo yao. Tulibaki wawili, tuliendelea na mazungumzo yetu. Nilijiuliza, inakuwaje vijana wale wana majina ya kienyeji, ina maana hawajabatizwa? Lakini mbona ni wakubwa sana? Nilimuuliza:-
"Vipi dada, ina maana hawa vijana hawajabatizwa, mbona wana majina ya kienyeji?
Bi Tamaa alikuwa kimya kwa sekunde kadhaa. Aliniomba radhi, nimpe dakika chache awatume vijana wakatafute mahitaji ya mchana. Baada ya kuwa amemalizana nao , aliketi na kisha aliniambia:-
"Hawa vijana wetu waliisha batizwa, wote wana majina yao. Lakini hawapendi kuyatumia. Baba yao alipo kuwa hai alikuwa anawaita majina yao ya ubatizo. Lakini tangu afariki baba yao, majina yao nayo yamekufa.
Hapo ndipo nilipo pata ufahamu kuwa alikuwa anaishi na bwana mwenye watoto hao. Lakini je marehemu mwenye watoto hao alikuwa ni mume wa ndoa au? Nilifanya ujasili wa kuelewa hilo. Bila kusita alifunguka:-
"Kaka, baada ya mimi kuondoka nyumbani, nilikutana na huyu marehemu mwenye watoto hawa. Tumeishi naye bila ndoa hadi anaondoka duniani.
Familia nzima ya ukweni kwangu hainitambui. Inanitaka niondoke niwaachie nyumba yao. Baadae nilikuja kujua kuwa nyumba hii ni ya mdogo wake amabye naye ni marehemu."
Maelezo hayo yalinitia simanzi sana, nilifikiria mengi sana ya kuweza kumsaidia, likiwemo swala la kisheria, lakini niliona litachukua muda mrefu pamoja na gharama kubwa zitatumika. Nilimpa ushauri kwa nini asirudi nyumbani? Lakini alinijibu ya kwamba:-
"Nyumbani kaka, nina miaka chungu nzima imepita sina masiliano na mtu yeyote, naogopa kurudi. Kingine ni familia hii ya ukweni ilinipa muda wa mwaka mmoja tu niwe nimeodoka. Kwa sasa bado nina miezi sita tu ya kuwa hapa. Nitafanya nini?"
Maelezo yake yalinitia uchugu sana. Nilifikiria jinsi ya kumsaidia. Nilikumbuka wito wa baba yake Mzee Busa kwamba arudi nyumbani. Nilimwahidi awe na amani, avumilie ndani ya miezi miwili. Nitarudi kumchukua mimi mwenyewe na mambo yote mimi nitamsimamia.
Alifurahi sana nilipo mhakikishia hilo. Tulikaa na kushusha dua mbili tatu. Kesho yake niliodoka kkurudi mjini kujiandaa na safari ya kurudi Shinyanga.
Nilipofika Shinyanga, nilifika nyumbani kwa Mzee Busa, nilimweleza hali halisi niliyo mkuta nayo Bi.Tamaa. Nilimpa uhakika ndani ya miezi miwili nitakwenda kumchukua mimi mwenyewe na nitamrudisha nyumbani. Nilimhakikishia hilo kwa kuwa nitakuwa katika kipindi cha likizo. Hivyo nitakuwa na wasaa mkubwa wa kulitekeleza hilo. Alinishukuru sana.
Siku, zinahesabika. Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Mwenyezi Mungu alinijalia muda wa likizo yangu ulikuwa tayari umetimia. Jambo la kwanza kulishughulikia lilikuwa ni la Bi Tamaa.
Nilfunga safari ya kwenda Mwanza. Naikumbuka siku niliyofika nyumbani kwake huko Igoma ilikuwa ni Ijumaa jioni. Sikumpa taarifa juu ya safari yangu, wala Mzee Busa pia sikumtaarifu.
Kwa bahati nzuri nilifika Igoma, sikutaka kupitia nyumbani kwa jamaa yangu, bali nilienda moja kwa moja nyumbani kwa Bi.Tamaa. Ilikuwa majira ya jioni kama saa kumi na moja hivi. Nilimkuta anapembua mchele, nadhani ilikuwa ni maadalizi ya chakula jioni.
Alinilaki kwa furaha, kwani hakutegemea ujio wangu kwa siku hiyo. Alinikaribisha hadi ndani, tulipeana habari za wakati uliopita na mambo kadha wa kadha. Vijana nao walikuwa wameisha rudi kutoka kwenye matembezi yao.
Baada ya kupata chakula cha jioni hiyo, nimwambia makusudi ya safari yangu. Hivyo basi aanze kufunga vitu vyake vizuri na ndani ya wiki moja tuwe tumeisha ondoka. Alifurahi sana kupata taarifa hiyo.
Siku iliyofuata asubuhi na mapema, bado nikiwa katika chumba nilichokuwa nimelala, nilimsikia anaongea na wanae. Bi Tamaa alimwita mwanae Love kisha alimuuliza:-
"Mwanangu, umeandaa nguo zako utakazo vaa kesho unapo enda Kanisani?"
Love alimwitikia mama yake Bi Tamaa:-
"Ndiyo mama nimeisha andaa."
Bi.Tamaa aliwageukia watoto wa kiume, kwanza alipunguza sauti ya Radio, kisha alimuuliza mwanae Kibonge iwapo nao wamejiandaa. Alimjibu kuwa:-
"Sisi mama tumeisha jiandaa tangu jana, tupo timamu kwa kesho."
Nilitoka ndani ya chumba nilicho kuwa nimelala, niliketi sebuleni, sikumkuta yeyote pale sebuleni. Baadae kidogo Bi. Tamaa alirudi na kuketi kwenye sofa huku akikumbatia kitoto cha mto wa sofa. Aliwaita tena wanae, baada ya kumwitika wito wake, aliwaambia:-
"Wanangu mnisikilize, nataka niwaambie kitu."
Watoto wote kwa pamoja walimwitikia kwa hali ya kutoshangaa:-
"Tunakusikiliza mama."
Aliwakumbusha kuhusu kifo cha baba yao aliyefariki mwaka mmoja na nusu uliopita. Aliendelea kuwajulisha jinsi familia ya baba yao isivyo mthamini yeye, na inamtaka aondoke ndani ya miezi michache iliyobaki. Hivyo nataka niwaambie kwamba:-
Nimefikiria tufanye shauri moja. Mimi nina kwetu, itabidi twende."
Love alimuuliza mama yake huku akiwa na wasiwasi fulani hivi:-
"Kwenu wapi mama?"
Bi Tamaa alimjibu mwanae kwa sauti ya upole na ya chini kabisa:-
"Ni nyumbani kwa wazazi wangu, kama mlivyo nyie hapa kwa sasa."
Kahindi alitaka kufahamu maeneo ya nyumbani kwao na mama yao. Bila kuwa na shaka Bi Tamaa alimjibu mwanae kuwa:-
"Kwetu ni Shinyanga, sehemu moja inajulikana kwa jina la Ibenzamata."
Watoto walionekana kuchanganyikiwa, kwani tangu baba yao akiwa hai, hawakuwahi kusikia wala kusimuliwa kuwa, mama yao ana wazazi. Mtoto wa mwisho ambaye ni Kitinda alimuuliza mama yake kwa unyonge sana:-
"Mama tutaondoka lini?"
Bi Tamaa alimjibu mwanae kuwa:-
"Nategemea uwezo wa Mungu. Ikiwezekana kabla ya Jumapili ijayo tutaondoka."
Mtoto wake Kibonge nae hakuwa nyuma kutaka kujua kuhusu nyumba na vitu itakuwaje? Bi Tamaa alimtuliza mwanae kisha alimjibu:-
"Shangazi yenu atakuja kuishi hapa. Ila vitu vyote tutakavyo weza kuchukua tutaondoka navyo."
Mama watoto huyu alizidi kuwafahamisha wanae kuwa, safari yao itasimamiwa na mimi mjoba wao. Wote kwa pamoja walinishukuru kwa kuwapa msaada huo.
Watoto wote waliafiki wazo la mama yao, walikubali kuondoka na mama yao. Siku iliyofuta niliondoka nikaenda zangu mjini kwa ajili ya kutafuta vifungashio vya mizigo. Nilikutana na dereva wetu, nilidhani labda naye yuko likizo na kumbe haikuwa hivyo.
Dereva huyo aliniambia kuwa analo gari kubwa la mizigo, ni jana tu alikuwa ameleta mizigo ya afisa mmoja. Hivyo anategemea kuondoka kurudi siku ya Alhamisi. Nilimuomba anipe msaada wa usafiri. Alikubali lakini alinishauri, tufanye juu chini Jumatano jioni nimfuate, ili mizigo yote tuipakie siku hiyo. Ifikapo Alfajiri ya saa kumi tuanze safari yetu.
Nilifanya haraka kurudi Igoma ili niwasaidie katika kufunga mizigo. Nilimpa habari hizi Bi.Tamaa pamoja na wanae. Ilipofika Jumatano mchana, asilimia kubwa tulikuwa tumeisha maliza kufungasha. Nilimfuta dereva kama alivyo kuwa ameniahidi. Baada ya chakula saa mbili usiku tulianza kupakia kwa bahati nzuri gari lilikuwa ni kubwa tani kumi, hivyo tulipakia kila kitu.
Dakika tano kabla ya kuondoka, Bi.Tamaa alimpigia simu shangazi yao wanae, alimjulisha kuondoka kwake na kwamba nyumba ipo wazi. Alimalizia na neno Kwa la 'kwa heri wifi ya kuonana.'
Tulifunga safari iliyotuchukua masaa matatu hivi hadi tulipofika Ibenzamata mkoani Shinyanga. Saa mbili kasoro ya asubuhi tulikuwa tumeisha bisha hodi kwenye mji wa Mzee Busa. Mara nilimsikia Bi.Tamaa anapiga kelele za:-
"Aaaa, nyumba yetu naikumbuka sana."
Tuliitoa mizigo ndani ya gari tulisaidiwa na mwenye gari na wale tulio wakuta hapo nyumbani. Nyumbani kwa Mzee Busa kulikuwa na mshangao, Ustadhi na wadogo zake hawakuwajua wao ni akina nani. Lakini baadae kumbukumbu zilimwijia na alimkumbuka kumbe ni dada yake. Kulikuwa na shangwe za hapa na pale huku wakikumbatiana na kusikika wanaongea:-
"Lu lu lu luuuuu dadaaa Kulu, le le leeee mdogo wangu Adul."
Watoto wa Bi. Tamaa walishikwa mikono na wenzao, wegine walibebana juu juu kwa upendo na furaha. Mke wa Ustadhi alibaki kashangaa asijue cha kufanya. Walikaribishana ndani kwa shangwe. Ustadhi alimwambia mkewe:-
" Bi Fati, huu ni ugeni, hebu wapumzike kwanza, wamechoka. Fanya utaratibu wa chakula, baadae tutaongea nao."
Baada ya chakula cha usiku, walikaa na kipeana taarifa mbali mbali. Lakini Ustadhi alikuwa anasita kumwambia dada yake Bi Tamaa. Akiwa katika hali hiyo mara Bi Tamaa alimuuliza kaka yake Ustadhi:--
"Kaka, baba na mama wako wapi?"
Ustadhi alipatwa na kigugumizi asijue ni jibu gani ampe dada yake. Ilibi Bi Tamaa awe mkali kidogo ndipo Haya alitoa jibu kwamba:-
"Baba na mama wapo Kolandoto, shangazi yetu kafariki juzi."
Tamaa alishituka sana, kilio kilimtawala bila matarajio. Watoto wake walipomuona mama yao analia na kutaja shangazi. Hawakujua ni shangazi yupi anaye mtaja. Wao walichukulia ni dada wa baba yao. Nao walihuzunika na kulia, walifahamishwa kuwa yule ni bibi ama Nyanya yao, mzaliwa wa tumbo moja na Babu yao kwa upande wa mama yao.
Ustadhi na ndugu zake walijitahidi kumtuliza, majirani nao walifika wakidhani kuna msiba. Baadae alitulia na mazungumzo yakaendelea. Bi Tamaa alitakujua sababu ya kifo cha shangazi yake. Ustadhi alimweleza dada yake:-
"Siku hiyo shangazi alitoka kusali msikitini, akawa anadai kichwa kinamuuma, asubuhi yake akafariki."
Baada ya maelezo hayo, Bi Tamaa alimshukuru Mungu na kusema:-
"Bwana asifiwe."
Watoto na mama yao waliitikia "Amen." Bi Tamaa alisherehesha kwa na kusema:-
"Yote ni kazi ya Mungu, tulimpenda, yeye kampenda zaidi."
Wote kwa pamoja walitakiana usiku mwema, hadi hapo kesho0 Mola akiwajalia.
Sura ya "2"
Kesho yake kama kawaida waliendelea na shughuli za nyumbani na shambani. Usiku baada ya kula chakula, waliketi tena kuendelea na mazungumzo yao, Ustadhi alihoji:-
"Dada, hujanitambulisha kuhusu hawa watoto."
Bi Tamaa alimwambi kaka yake kwamba asijali wala asiwe mashaka. Ndipo alipo anza kumtabulisha:-
"Kaka, hawa wote ni wapwa zako ni watoto wangu mimi dada yako. Huyu ni Kibonge, akafuatia Love, akaja Kahindi na mwisho ni Kitinda"
Ustadhi alitaka kujua shemeji yake yaani baba wa watoto hao ni wapi aliko. Dada alimjibu kaka yake:-
"Shemeji yako ni kama yalivyotokea kwa Shangazi; ni mwaka na nusu tangu afariki."
Ustadhi hakuishia hapo tu, aliendelea kutaka kufahamu, muda wote wa ukimya huo alikuwa amejificha wapi? Bi Tamaa alimjibu kaka yake:-
"Mimi baada ya kuondoka hapa nyumbani, nilikutana na marehemu baba watoto wangu, ndiye aliye nihodhi kwake huko Mwanza. Huko ndiko nilikotokea kwa sasa."
Siku kadhaa zilipita na hata siku moja iliyo kuwa ni Jumapili, siku ambayo Bi Tamaa na wanae huwa hawakosi kwenda Kanisani. Kibonge alimuuliza mama Bi Tamaa iwapo wataenda Kanisani. Lakini mama alimjibu:-
"Leo mwanangu sijisikii vizuri, ngoja nimwambie jirani yetu mama Helena ili muongozane nae."
Kibonge alimsisitiza mama kuwa amwambie mama Helena wawahi misa ya pili. Bi Tamaa alimuomba mama Helena, kwa bahati nzuri alimkuta yupo hatua za mwisho za kuelekea Kanisani.
Kibonge aliondoka na wadogo zake wote waliambatana na mama Helena. Baada ya ibada, walirudi nyumbani wakiwa na furaha huku wakilisifia Kanisa lilivyo kubwa na zuri.
Muda mchache ulipita baada ya kula chakula cha mchana. Kibonge aliwaita ndugu zake yaani Love, Kahindi, na Kitinda. Walitaka kujua alichowaitia. Lakini aliwaambia watulie. Kisha aliwauliza:-
"Hebu niambieni ndugu zangu, tangu tumefika hapa, mmegundua nini? Kitu gani kilicho tofauti na huko tuliko toka?"
Wote kwa pamoja walimjibu kaka yao, kuwa wao, hawajagundua chochote, wala hawajaona tofauti yoyote. Hapo ndipo alipowauliza:-
"Mama hatukuwa nae Kanisani siku ya leo, mnajua ni kwa nini?"
Love alimjibu kaka yao kwamba, mama yao aliisha sema hajisikii vizuri. Lakini kaka yao alilikanusha hilo. Ila aliwaelewesha kuwa:-
"Usemayo ndugu yangu ni sawa, lakini mama hajawahi hata siku moja kuikosa ibada ya Jumapili!"
Wote tena kwa pamoja wakiongozwa na Kahindi, walihoji ni kitu gani kaka yao anachotaka kuwaeleza? Kaka yao alianza kutoa darasa, aliwaambia:-
"Sasa nisikilizeni nilicho kigundua mimi, mjomba wetu ambaye ni kaka yake mama yetu, kama mulivyo sikia anaitwa 'Ustadhi'. Mbali na hawa wengine, inawezekana wanayo majina ya kiimani. Sasa kwa nini mama yetu awe muumini wa ki-Kanisa? "
Love alionekana kuwa ana wingi wa masikitiko kwa yale aliyo yaelezea kaka yao. Kisha nae aliuliza:-
"Sasa ina maana kuwa, mama nae ni Muislam? Sasa ilikuwaje ashike ibada za ukristo?"
Kibonge ilimuiya ugumu, hasa pale wadogo zake alipo waona kuchanganyikiwa. Hata hivyo alijitahidi kuwaelewesha. Pamoja na hayo Love aliuliza:-
"Sasa jamani tufanye nini?"
Hata hivyo penye wengi hakiharibiki kitu. Kitinda nae alitoa ushauri wake:-
"Katika kuwaza kwngu, naomba tufanye subira hadi siju ya Ijumaa tuone. Je, mama ataenda msikitini?"
Kila mmoja alikuwa ananung'unika lwake, mwishoe Kahindi nae aliuliza iwapo mama yao atakwenda ama asiende Msikitini itakuwaje, ni nini kitafuata? Kitinda alijitahidi kuwaweka sawa kwa kuwaeleza kuwa:-
"Jamani, tukiisha ona hivyo, tusimuogope mama, tutamuuliza atupe sababu iliyo watofautisha yeye na mjomba, au ilikuwaje akaangukia upande huu wa pili.?"
Wote kwa pamoja waliafiki wazo la mwenzao. Baada ya siku Ijumaa ilifika. Wote walikuwa na shauku ya kutaka kuona kulikoni. Lakini Bi Tamaa hakwenda Msikitini, isipokuwa Ustadhi na familia yote, walikwenda Msikitini. Ndipo hapo Kitinda alipowaambia na kuwauliza:- Nadhani kila mmoja wetu kajionea mwenyewe na jibu tayari tunalo. Sasa mnasemaje?"
Love alitoa wazo ambalo kwa upande mwingine wanaweza kupata ukweli wa mambo. Aliwaambia wenzake:-
"Mimi ninaona ni vizuri tumwambie mjomba Ustadhi kwamba, tufanye majadiliano ya kifamilia huenda itatusaidia."
Kahindi nae alikuwa analo la kuhoji. Yeye hakuona kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Hata hivyo aliuliza:-
"Jamani, hivi cha msingi ni nini tunachotaka kujua?" Love hakuchoka kuwafahamisha ndugu zake. Aliendelea kuwaambia:-
"Sikilizeni, shabaha yangu ni kutaka kupata ufahamu wa upande wa pili, pia utatuondolea dukuduku tulilo nalo."
Kitinda nae hakuwa mkimya, ingawa alikuwa hajaongea kipindi. Alitoa nae maoni yake kuwa:-
"Ukweli ni kwamba, hata mimi nakubaliana na dada Love, kwani itakuwa na manufaa katika maisha yetu na vizazi vijavyo."
Mwisho walikubaliana kufanya mazungumzo na mjomba wao, na wakae kama familia. Kibonge alichukua jukumu hilo la kumwalifu mjomba wake kama walivyo kubaliana.
Mnamo majira ya jioni kama saa kumi na mbili hivi, mzee Busa na mkewe waliwasili safari yao waliyo kuwa wameenda. Baba na mwana walikumbatiana kwa furaha, na kisha mama na mwana walifanya hivyo hivyo huku kamasi na machozi ya furaha yakiwatoka.
Walizungumza hili na lile, hapakuwa na jambo lolote labda la huko nyuma lililo fanyika kimakosa. Yote waliyasamehe na kusameheana maisha yakaendeklea.
Mzee Busa alimwita mwanae Tamaa, alimwabia amletee wajukuu zake awaone vizuri. Lakini kabla ya kitendo hicho, mzee huyo alinipa hongera nyingi na shukrani tele, na kwamba hana cha kunilipa bali Mwenyezi Mungu atanilipa. Alinishukuru sana nilimrejeshea mwanae aliye toweka kwa miaka chungu nzima.
Tamaa aliwakusanya wana, akawapeleka kwa Babu yao, aliwatanbulisha wamfahamu babu yao. Kisha alianza kumtajia majina ya wanae. Alipomaliza, Mzee Busa alitaka kufahamu baba wa wajukuu zake, mbona hapo hamuoni, hakuja naye?
Tamaa alimsimulia baba yake A - Z kuhusu baba wa watoto. Baba yake alisikitika sana kusikia habari hizo. Alimwambia mwanae, aondoe shaka, ili mrdi amerudi salama Mwenyezi Mungu ndiyo mpangaji wa kila kitu. Aliendelea kusema:-
"Namshukuru Mwenyezi Mungu, umerudi ukiwa na wajukuu zangu. Ila haya majina hayaleti raha kuyatamka. Sasa nitafanya hivi, huyu Kibonge nitamwita 'Kibon', huyu Love litabaki hivyo hivyo. Kahindi atakuwa Kahin na huyu wa mwisho atakuwa Kitin badala ya Kitinda. Mnaona yanavyo pendeza kutamka hata kuyaandika?"
Wajukuu walimfurahia babu yao, kila mmoja walikuwa wanamshika shika babu yao kichwani, wengine walifurahia mvi zake. Ilifika siku waliyo kubaliana kuweka kikao cha kifamilia. Kibon alimwambia mjomba wake:-
"Mjomba, kwa niaba ya wenzangu, nakuomba kabla ya Jumapili, siku moja wapo tukae kama familia, tuna yetu ya kuongea."
Ustadhi alipatwa hofu juu ya ombi hilo, alijiuliza maswali mengi lakini hakupata jibu. Aliishia kuuliza:-
"Labda ungenidokeza, maongezi hayo yatahusu nini ili nipate kujiandaa vizuri."
Kibon hakuwa mtu wa kuzunguka zunguka aliweka wazi bila kusita, alimweleza mjomba wake:-
"Mazungumzo yetu mjomba ni Uislam, sisi tumekulia kwenye ukristo. Itakuwa vizuri tukipata mawili matatu, itakuwa ni dira kwetu.
Mjomba aliitikia wito huo, aliahidi kesho yake baada ya chai watakaa. Tena bahati nzuri, Babu yao yupo. Mambo yatakuwa mazuri tu.
Sura ya "3".
Kama walivyo kubaliana, baada yakipindi cha chai walikutana na kukaa kama kikao cha familia. Kuluth alitoa kauli:-
" Tunakusikiliza."
Ustadhi aliwatoa wasiwasi wapwa zake, kwamba wawe huru kuzugumza lolote bali pawe na heshima. Aliongeza kusema:-
"Hapa jamani tupo kama familia, Kibon na wenzake, wameniomba tukae na tuongee machache, na hasa kuhusu Uislam kwani wana haja ya kujua."
Adul alikuwa kimya kwa muda mrefu, wakati wote alikuwa anawasikiliza, ila aliuliza swali:-
"Kwani tatizo ni nini?"
Kwa kuwa Kibon alipewa jukumu hilo, hivyo alikuwa na kazi kubwa sana ya kutoa ufafanuzi. Aliwaambia kuwa:-
"Ndugu zangu, tatizo halipo, sisi tunaomba kuufahamu Uislam, sisi tumelelewa ndani ya Ukristo. Leo hii tupo kwenye wigo wa Uislam, kibaya zaidi Uislam hatuujui. Itakuwa vyema tukitoka gizani."
Ustadhi aliwasikiliza kwa makini, alikuwa anatafakari aanze na kipengere kipi. Alimtaka Kibon amfahamishe kuwa wataanza na kipengele gani. Naye Kibon alimjibu:-
"Mjomba, niliwahi kusikia, kuna mijadala kati ya Wakristo na Waislam juu ya imani zao. Kwani ilikuwa ni kwa sababu gani?"
Ustadhi alitabasamu, alimwangalia Kibon kisha akamgeukia Adul akamkazia macho, akamwambia:-
"Haya tena, mijadala yenu mjibu mwanao." Adul alijibu haraka haraka:-
"Kwa sababu tunaamini, Muumba ni mmoja tu."
Ustadhi naye hakubaki nyuma alizidi kusema:-
"Kwa nyongeza ni kwamba, Mitume mbalimbali aliowaleta hapa duniani ni Muumba."
Kulut nae hakubaki nyuma kutoa anacho kifahamu, alisema:-
"Vile vile sisi Waislam tunaamini kuwa Yesu ni Masihi na ni neno la Mungu, ingawa Mayahudi wanamkana."
Ustadhi alikuwa mahili kwa kujieleza, hakuwa tayari kuonekana amechoka ama kashindwa. Bali aliendelea kuwaelesha kwamba:-
"Katika Qur'an sura ya 3:4 inasema: (Kumbukeni) walipo sema Malaika: Ewe Mariam, Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za kumzaa mtoto bila ya mume, bali kwa kutamkwa). Jina lake ni Masihi Isa, mwana wa Mariam, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na ni miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu."
Kibon na wenzake walikuwa wakitazamana mara kwa mara na hata kumwangalia mama yao. Kibon alimuuliza Haya:-
"Mjomba, nimewahi kusoma mahali fulani kwamba, mijadala mingi imewahi kufanyika nchi za ulaya, Australia, Marekani na Canada pia Vetican katika miaka ya karibuni. Sasa, kwa nini basi mijadala hiyo isifanyike enzi hizo iwapo Ukristo una takribani miaka elfu mbili na Uislam ni zaidi ya karne kumi na nane?"
Ustadhi alikaa kimya kwa muda wa sekunde kadhaa. Nadhani alikuwa anatafuta jibu la kumtosheleza Kibon pamoja na wenzake. Aliinua kichwa, akajitengeneza kwenye kiti alichokalia. Akamnyooshea mkono Kibon kisha akamjibu:-
"Tafadhali nielewe vizuri, karne tatu au nne za nyuma, Waislam walio kuwa Afrika na Asia, walikuwa mikononi mwa ukoroni wa Mwingereza, Mjerumani, Mfaransa na Mreno pia Mholanzi."
Kibon alikuwa bado hajamwelewa Ustadhi alicho kidadafua. Hata hivyo Ustadhi alimfahamisha Kibon kuwa alikuwa bado hajamaliza, hivyo aliendelea kutoa maelezo:-
"Wakati huo wamisionari walitumia mbinu za kuwaingiza Waislam kwenye Ukristo kwa kisingizio cha kuwapa matibabu, nguo na vyakula nk. Hata hivyo mafanikio yalikuwa ni kidogo. Wale walioingia Ukristo ni kutokana na ufahamu na imani yao ya kwamba umewapelekea ustaarabu na maendeleo kielimu, ambazo zilikuwa ni fikra potofu."
Kahin hakuelewa aliposikia neno potofu kwa nini kulikuwa na fikra potofu? Hivyo alitaka kufahamishwa. Ustadhi alizidi kuwaelewesha:-
"Jamani, nasema fikra potovu kwa sababu. Maendeleo yalipatikana baada ya Kanisa kutenganishwa na dola huko Ulaya, kwani Waislam walihamia nchi za magharibi baada ya vita vya pili ya dunia. Hivyo Waislam walifanywa kuwa karibu sana na Wakristo." Kibon baada ya kuwa kimya kwa muda, aliwageukia ndugu zake wengine na kuwauliza kuwa mbona wao hawaulizi? Love aliyekuwa kimya kwa muda mrefu, ghafla alikohoa kikohozi kilicho ashiria kuwa alikuwa amepitiwa na usingizi. Ndipo alipo uliza:-
"Mjomba, kwa nini basi mijadala siku hizi inafanywa na wahubiri wa Kikristo wenyewe?"
Ustadhi hakuwa na uchovu wala kukerwa na maswali ya wapwa zake. Alijitahidi kuwaelesha kadri ya uwezo wake. Aliendelea kusema:-
"Kwa mujibu wa Qur'an ndugu zangu, sura ya 5:82 inasema hivi: Hakika utawakuta walio maadui zaidi na watu wengine kwa Waislam ni Mayahudi na Mshirikina, na utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislam ni wale wanaosema: 'sisi ni Wakristo.' Hii ni kwa sababu wapo miongoni mwao wanavyuoni na wacha Mungu, na kwa sababu wao ni Wakristo hawatabakari wakijua haki kuifuata."
Kitin alipata ugumu wa kuelewa kutokana na sura hiyo. Alimwambia mjomba Ustadhi kuwa yeye bado kabisa hajapata kitu yaani hajaelewa. Ustadhi alitumia kila mbinu kuwaelesha, aliendelea kusema:-
"Kwa kuwaeleza kwa maneno matupu hamuwezi kunielewa vizuri. Ni hivi, baadhi ya madhehebu ya Kikristo yanakubali kuwa Muhammad (s.a.w) ni kizazi cha Nabii Ishmail kwa mtoto wa pili Kedari. Sasa ukitaka kujua kwa usahihi habari hizi, pata vitabu vifuatavyo:-
1. The Davis Dictionary of the Bible 1980
2. Agano la Kale: Mwanzo 25:13.
3. The International Standard Bible Encyclopadia- nukuu ya A.S. Fulton.
4. Smith Bible Dictionary."
Bi Tamaa alikuwa kimya, hakuweza hata kuchangia lolote. Mara kwa mara hakuchoka kuinuka na kutoka nje. Nadhani alikuwa na wasiwasi kuwa huenda akaulizwa mambo kadhaa wa kadhaa. Ghafla aliuliza iwapo yeye anaweza kuwa Mwiislam. Ustadhi alimjibu:-
"Haswaa, utakuwa unarejea kwenye Uislam."
Jibu hilo halikumuweka sawa Kibon. Alishindwa kuelewa, atakuwa anarejea vipi kwenye Uislam wakati yeye ni Mkristo? Ghafla Kulut alidakia na alizidi kumuelewesha:-
" Ni kwamba, mtu yeyote anapozaliwa, huwa ni Mwiislam. Wazazi wake ndio wanao mbadilisha afuate Uyahudi, Ukristo na imani za kishirikina."
Mazungumzo yalikuwa magumu, lakini ni mazuri, hakuna aliyeonesha kuchukizwa, bali ni tabasamu lilitanda kwa wote miongoni mwao. Hapo hapo Kitin nae aliuliza:-
"Iwapo Uyahudi, Ukristo na Uislam zinatokana na Muumba mmoja, sasa kwa nini basi zitofautiane?" hali kdhalika Ustadhi alichukua nafasi ya kulidadafua swali la Kitin. Alitoa ufafanuzi kuwa:-
"Kutoka Mtume Adamu mpaka Mtume Muhammad (s.a.w) walikuja na ujumbe mmoja tu. Wanadamu wote wajisalimishe kwa Allah (s.w)"
Adul aliona jibu hilo lina upungufu kiasi fulani. Upungufu huo aliukamilisha kwa kusema:-
"Tuelewe kwamba, neno kujisalimisha, kwa Kiarabu ni 'Islam' pia ni 'Aman' baina ya Muumba na viumbe vyake."
Ustadhi nae aliona bado kuna mapungufu ya jibu hilo, alijazia kwa kuwaelesha zaidi kwamba:-
"Kwa ufafanuzi zaidi, jina hilo la Islam, limetokana na Muubaji mwenyewe kama ilivyo Qur'an sura ya 5:3 isemayo: Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu, na nikakuchagulieni Islam iwe dini yenu (njia yenu ya maisha)."
Muda ulizidi kuwa mwingi, ilikuwa ni saa saa saba na nusu. Ustadhi aliwataka wapumzike kwanza mpaka hapo watakapo pata chakula cha mchana ndipo waendelee na mazungumzo yao.
Sura ya "4".
Kipindu cha kupata cjakula cha mchana kilikamilika, kila mmoja akiwa na nguvu na mawazo mapya. Walikaa na kuendelea na mazungumzo yao. Love alikuwa wa kwanza kuuliza swali:-
" Mimi nakuona mara nyingi unanukuu katika Qur'an. Sijaona umegusia Biblia?"
Ustadhi hakuwa na shaka yoyote kuhusu Biblia inawezekana anao ujuzi wa vitabu hivi, alimjibu moja kwa moja:-
"Hapana Love, huko ndiko niendako ili muione tofauti. Sasa basi katika Biblia hakuna neno Uyahudi au Ukristo, na hata kwenye kamusi ya Biblia. Wala Mitume wa Uyahudi hawakutaja neno Uyahudi. Yesu hakudai kwamba ameleta Ukristo na hakujiita mkristo."
Adul naye aliona ni vyema ashereheshe anacho kifahamu. Ili wapate ufahamu mkubwa zaidi, alisema:-
"Hata hivyo ndugu zangu, neno Mkristo katika Agano Jipya limetajwa mara tatu. Kwanza limetajwa na Alikuwaapagani kisha Wayahudi wa Antionkia yapata miaka arobaini."
Ueleweshaji uliendelea kwa amani kubwa, kwa kuheshimiana. Kulut aliongeza na kusema:-
"Pia Matendo ya Mitume 11:2. Inasema kuwa 'na wanafunzi waliitwa Wakristo wa kwanza hapo Antiokia."
Maswali na majibu yaliendelea kwa kila mmoja kile anacho kielewa kwa ushirikiano mkubwa. Lakini Kibon alijitosa kuwafahamisha kuwa hakuelewa na alichokisoma kina maanisha nini alisema:-
"Subirini niwaambie, kuna siku sikuelewa ina maanisha nini niliposoma Matendo 26:28 inasema: Agripa akamwambia Paulo, kwa maneno machache wadhani kunifanya mimi kuwa Mkristo?
Ustadhi aliyekuwa ndio baba mwenye mji kila kitu kilikuwa mikononi mwake. Alitumia hekima kubwa katika kuongoza mazungumzo yao. Aliwaelewesha kuwa:-
"Neno Ukristo kwa mara ya kwanza na maadui na sio marafiki. Kisha Petro katika walaka wake wa kwanza 4:16 amelitaja alipokuwa anawafariji waumini wake."
Baada ya kuonekana mazungumzo yanakuwa makali, vitabu vitakatifu vilikusanywa ili kila litakalo tajwa basi lionekane ndani ya vitabu hivyo.
Love alichukua Biblia akafunua baadhi ya kurasa, alizisoma kimya kimya, alionekana anakunja uso kama kuashiria kwamba kuna kitu hakielewi. Hakudumu na ukimya bali alimuuliza Ustadhi:-
"Iwapo Mitume wote walikuja na neno moja la Islam. Mbona Nabii Ibrahim ni Myahudi?"
Ustadhi alimuuliza Love aliye mwambia hivyo ni nani? Alimjibu kuwa ndivyo wanavyo fundishwa na Biblia nayo inathibitisha. Katika kumuweka sawa alimwambia afunue Biblia Mwanzo 11:31 kisha asome na wasikie wote. Alifunua Biblia kisha alianza kusoma:-
"Tera akamchukua Abraham mwanae, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanae, Sarai mkewe mke wa Abraham mwanae, wakatika wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kaanani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko."
Ustadhi aliendelea kufafanua maandiko hayo kuwa:-
"Unaona sasa, Abraham amezaliwa Uru wa Wakaldayo siyo Myahudi. Uru wa Wakaldayo ilikuwa Mesopotamia, kwa sasa ni sehemu ya Iraq, Abraham ni Mwarabu. Neno Myahudi limekuja baada ya kuja Yuda, kitukuu cha Nabii Abraham."
Ustadhi aliweka juhudi zake zote ili mradi wapwa zake waelewe. Alimwmbia Love aendelee kusoma Mwanzo 12:4-5, alisoma:-
"Nae Abraham alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipokaa Parani....nao wkaingia nchi ya Kaanani."
Ustadhi aliendelea na ufafanuzi zaidi kwa kusema:-
"Unaona sasa, Abraham alihamia Kaanani akiwa na umri wa miaka sabini na tano na alikuwa mgeni. Mpaka hapo unasemaje?"
Ustadhi baada ya hapo alimuomba Love aendelee na Mwanzo 17:8 ambayo Love alisoma:-
"Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kaanani kuwa miliki ya milele, nami nitakuwa Mungu wao."
Usitadhi alimuonya Love kuwa ameyaona hayo? Alimtaka tena aendelee na Mwanzo 14:13 nae aliisoma:-
"Mtu aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abraham Mwebrania."
Ustadhi aliendelea kumwelewesha Love, alimwambia:-
"Hebu niambie sasa, takuwaje useme Abraham ni Myahudi wakati Biblia inamwita Mwebrania? Tena atokaye upande wa pili wa Farati; mwenye mahusiano na Eba uzao wa Shem?"
Ustadhi alimuomba Love amalizie kusoma Mwanzo 32:28.
"Akamwambia jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu na watu, nawe umeshinda."
Ustadhi aliendelea kumfafanulia Love kwamba:-
"Abraham alikuwa Mwebrania, kizazi cha Yakobo walikuwa ni Waisraeli waliogawika makabila kumi na mbili. Yuda akaitwa Yahudi jina la utani, ndiyo ikawa asili ya kizazi cha Yuda kuitwa Wayahudi. Kwa kukuelewesha zaidi na ufahamu Musa alikuwa nani, endelea kusoma Kutoka 6:16-20"
Love aliendelea kusoma na wenzake walikuwa wanafuatilia ndani ya Biblia zao. Alisoma hiyo Kutoka 6:16-20:-
"Na hayo ndiyo majina ya wana wa Lawi, sawasawa na vizazi vya vyao, Gereshoni na Kohathi, na Merari.....Na wana wa Kohathi ni Amramu...... Huyo Amramu akamuoa Yokobedi ndugu ya baba yake, naye akamzalia Harun na Musa."
Ndipo tena Ustadhi aliendelea kutoa ufafanuzi mzima kwa kusema:-
"Umeelewa sasa Lucia? Musa hakuwa Myahudi kwa kuwa si katika uzao wa Yuda, bali anatokana na uzao wa Lawi. Musa alikuwa mtoa sharia Torati na shria kwa wana wa Israeli."
Baada ya hapo Love alimuomba mjomba Ustadhi aendelee kufafanua yote yaliyo baki. Hata hivyo kutokana na muda mwingi alioutumia kufafanua maandiko, alimtaka Adul aendelee. Nae alianza kwa kusema:-
"Haya tuendelee, lakini kipimo chetu ni Qur'an. Tunasoma Biblia na kukosoa chuki zilizo pandikizwa kwa Wakristo na Wayahudi kwa mnasaba wa Qur'an. Ni kitabu cha mwisho kilicho teremshwa, hakijaharibiwa wala kuchafuliwa kwa kuongezwa ama kupunguzwa yaliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe."
Adul alipo maliza kutoa maneno hayo, alimuomba Kulut kusoma Qur'an sura ya 2:2 na sura 15:9, alisoma kwa sauti:-
"Qur'an sura 2:2. Hiki ni kitabu kisicho kuwa na shaka ndani yake. Qur'an sura ya 15:9. Hakika sisi ndio tulioiteremsha Qur'an na hakika sisi ndio tutailinda dhidi ya uchafuzi."
Adul alianza kusherehesha aya hizo kwa kusema:-
"Huu ni ukweli ulio thabiti, kwani zaidi ya miaka elfu moja na mia nne imeshipita hakuna hata neno moja katika Qur'an lililo badirishwa, ingawa kuna jitihada za kuchafua mafunzo ya Qur'an, lakini imeshindikana. Vitabu vioivyo chafuliwa kwa kupunguzwa, kuongezwa au kubadilishwa sehemu kadhaa katika vitabu vya asili ambavyo ni Taurati, Injili, Zaburi na kadhalika."
Love alimsikiliza kwa makini Adul wakati anasherehesha mara alitoa swali, aliuliza:-
"Kwani Qur'an inasemaje juu ya Ibrahim na Musa kwa mambo ambayo yanalingana na Biblia kama ulivyosema?"
Adul alimtaka Kulut kwa mara nyingine tena asome Qur'an sura ya 3:65 na sura 3:67 pia Qur'an sura ya 2:140. Aliisoma:-
"Qur'an sura ya 3:65 inasema: Enyi watu mlio pewa kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili havikuteremshwa ila baada yake? Basi je, hamfahamu?
Pia Qur'an sura ya 3:67 inasema: Ibrahim hakuwa Myahudi wala Mkristo lakini alikuwa mwongofu, mtii na wala hakuwa katika washirikina.
Qur'an sura ya 2:140 insema: Mnasema nyinyi Wayahudi na Wakristo kuwa karibu n Ismail na Is haqa na Yaaqub na kizazi chake walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenezi Mungu? Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule afichae ushahidi alionao utokao kwa Mwenyezi Mungu si mwenye kugjafirika na hayo mnayoyafanya."
Baada ya kusomwa aya hizo, Adul alianza kuwafafanulia wapate kuelewa. Alianza kwa kusema:-
"Hapa ndipo tunaposema , Ibrahim na Musa hawakuwa Mayahudi wala Wakristo, jina la Mayahudi limetokana na Yuda na jina la Kristo limekuja kitambo baada ya Yesu kuondoka."
Love alimtupia nafasi ndugu yake Kahin apate nae kuhoji yale aliyo nayo. Dukuduku lake lilikuwa juu ya neno Allah. Kwake kilikuwa ni kigeni. Kwa nini neno Mungu au jwa lugha nyingine God lisitumike? Adu alitoa maelezo kwamba:-
" Unajua wasio Waislam huliona neno Allah ni kitu kigeni kwao, lakini mitume wote tangu Adam hadi Muhammad (s.a.w) wamelitumia."
Nae Ustadhi kwa mara nyingine aliendelea kuwaelewesha neno Allah kwamba:-
"Neno Allah ni maneno mawili ya Kiarabu. Al - Ilah, maana yake ni Mwenyezi Mungu. Kuiondoa herufi I unapata Allah."
Adul aliendelea kuwaelesha zaidi kuhusu neno Allah kwa kusema:-
"Katika sentenso za Kiarabu wakati mwingine hutamkwa 'Allaha' ambalo lina ukaribu na Eloha neno la Kiebrania lenye maana ya Muumba. Hivyo basi Mayahudi hulitumia kimakosa. Neno Elohim ambalo ni wingi wa neno Eloha na huleta maana ya Mungu zaidi ya mmoja."
Adul alitulia kidogo, aliwauliza iwapo wanakwenda wote pamoja. Walikubali kisha Adul aliendelea kufafanua zaidi.
" Neno Allah limefanana sana na q ambalo ni neno la Kiaramu alilolitumia Yesu lenye maana ya Mungu. Ukipata kitabu cha Encyclopedia Britanica 1980, soma chini ya neno Allah na Elohim. Pia neno Allah ni jina la Mwenyezi Mungu, haliwezi kubadilika na kuwa wingi, mke au mume. Nikiwa na maana ya kuwa, hakuna Mungu wa kiume wala wa kike kama ilivyo katika Kiingereza wanababaika kutumia neno God, nankuamini Mungu ni Yesu. Pia neno Muumba huwababaisha na kushikiria kuwa Yesu ni Muumba wa ulimwengu."
Sura ya "5"
Wote walikaa kimya na baadae walipeana dakika kumi za mapumziko na kisha wakaendelea moja kwa moja katika hoja iliyotolewa na Kitin kwamba:-
"Kwa nini mnapotaka kufanya ibada lazima utie udhu, halafu sijui kuna kusujudu na mengine mengi?"
Adul aliendelea na ufafanuzi wa hayo aliyo hoji Kitin. Aliwaambia kuwa, kwa wale wasio Waislam ni mageni kwao, lakini sio mageni hata kwa Mitume wote. Baada ya hapo akamwambia Kibon asome Biblia kutoka 40:31 - 32 inasemaje:-
"Inasema hivi, Musa na Harun na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake, hapo walipo ingia hema ya kukutania, na hapo walipo ikaribia madhahabu, walinawa kama Bwana alivyo mwamuru Musa." aliendelea kumwambia Kibon kuwa huo ndio udhu. Alimtaka tena amsomee Matendo 21:26 kisha Wakorintho wa Kwanza 11:5,6 na 13 halafu soma Zaburi 95:6 na Yoshua 15:4 baada ya hapo asome Wafalme wa Kwanza 18:42, Hesabu 20:6 na Mwanzo 17:3 zinasemaje:-
"Matendo 21:26 inasema hivi: Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siiu ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao.
Wakorintho 11:5,6 na 13 inasema hivi: Bali kila mwanamke asalipo au anapo hutubu, bila kufunika yaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliye nywele, maana mwanamke asipo funikwa na akatwe nywele. Au ikiwa mwanamke ni aibu kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe...... Hukumuni nyinyi wenyewe katika nafsi zenu. Je, mwanamke amuombe Mungu asipo funikwa kichwa?"
Zaburi 95:6 inasema hivi, njooni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele ya Bwana aliye tuumba.
Yoshua 5:14 inasema hivi, Yoshua akapomoka kiusouso hata chini ardhini, naye akasujudu......naye akasujudu.
Wafalme wa kwanza 18:42 inasema hivi, Naye Eliya akapanda juu hadi kilele cha Karmeli, akasujudu, kifudifudi, akainamisha uso hadi magotini.
Hesabu 20:6 inasema hivi, Musa na Harun wakatoka pale palikuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa Hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi, utukufu wa Bwana ukatawatokea.
Mwanzo 17:3 inasema hivi, Abraham akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia akasema........
Adul aliendelea kuwaelesha kwamba, mambo yote ya udhu, kusujudu na kurukuu yalifiatwa na Mitume wote. Isipokuwa Paulo ameweka mambo mengi ya uongo juu ya mafundisho ya Yesu. Hapo hapo Ismail nae akaingilia kati na kusema:-
"Naye Mungu akasema kumwambia Musa, usikaribie hapa vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali unaposimama ni nchi takatifu. Hii ni Kutoka 3:5 na Matendo 7:33."
Swala hilo halikuwa na mjadala tena, kila mmoja alilidhika, hata hivyo ilifuata hoja nyingine ambayo Kahin aliitoa isemayo kuwa: Yeye huwa anasikia na kusoma katika vyombo vya habari kuhusu HIJA. Kwamba huwa kuna kulizunguka jiwe takatifu huko Makka. Lakini hajapata kuona ndani ya Biblia.
Jambo hili limetajwa mara nyingi. Adul aliendelea kuwaelesha. Alisema kuwa, wasomaji wa Biblia wamelifumbia macho. Lakini Biblia imeainish kama ifuatavyo:-
1: "Yakobo alipokuwa akienda Padan Aramu aliota ndoto na asubuhi yake akajenga nguzo ya jiwe akaita Bethali, yaani nyumba ya Mungu. Mwanzo: 18:19.
2: "Baada ya miaka kupita Yakobo aliamrishwa aende Bethali. Yakobo aliondoa Miungu yote ya uongo kabla ya kwenda huko. Mwanzo: 35:4,14,15.
3: " Nguzo nyingine ilijengwa na Yakobo pamoja na mkewe Labani. Mwanzo: 31:45 - 49. Labani aliita Yegar Sahadutha, lakini Yakobo aliita Gileadi na Mispa.
4: "Yeftha aliweka nadhari kwa Bwana katika Mispa ya Gileadi. Aliposhinda vita dhidi ya wana wa Amon, alimchoma moto binti yake akiwa hai kama sadaka ya Bwana. Waamuzi: 11:29-39.
5: Wapiganaji mia nne elfu kutoka makabila kumi na moja ya Israeli waliapa mbele ya Bwana katika Mispa kuyaangamiza makabila ya Benyamini. Waamuzi: 20 na 21.
6: " Wana wa Israeli chini ya uongozi wa Samweli waliapa katika Mispa kuyavunja masanamu yao iwapo watawashinda Wafilisti. 1.Samweli: 7.
7: "Taifa zima la Israeli lilikusanyika Mispa wakati Samweli alipoteuliwa kuwa Mfalme wa Israeli. 1.Samweli:10.
Nimeyaelezea yote haya kuonesha uwazi kuwa hakuna Mispa yeyote duniani isipokuwa ile kongwe iliyopo katika mji mtakatifu wa Makka, iliyo jengwa na Nabii Ibrahim na mwanae Ismail, na Mtume Muhammad (s.a.w) aliye tokana na ukoo huo. Waislam ndio khasa wafuasi wa Mitume wote."
Mazungumzo yaliahirishwa, kwani usiku ulikuwa umeingia. Watoto walihitajika kuoshwa, kula na kulala. Hata wao watu wazima wenyewe walikuwa wameisha choka. Walikubaliana hadi siku nyingine watakayo iona inafaa.
Sura ya "6"
Zilipita siku kadhaa bila ya kufanyika mazungumzo yoyote. Hata hivyo mazungumzo yaliendelea tena baadabya kuwa wamekumbushana. Nae Abdul alisema:-
"Leo tumekutana tena, sasa tuendelee na hoja zetu. Lakini niwaulize swali. Kwa nini mnataka mjue yote hayo wakati hamtafuti ukweli?" Kibon aliyekuwa mwepesi wa kuelewa na kutoa maelezo, mara moja alijibu:-
"Mimi ni Mkristo nina uhakika wa imani yangu, lakini napenda kujua zaidi kuhusu dini zote mbili. Hata hivyo huwa naona kama vile nina kashifiwa ninapo visoma vitabu vilivyo andikwa na Waislam."
Adul alimuuliza Kibon iwapo amekerwa na waliyo yazungumza ikiw alijibu:-
"Yamenikera kwani imenisababisha nisipende kwenda Kanisani."
Adul alimuuliza tena kama ndivyo hivyo ni kwa nini anaendelea na mazungumzo haya? Kibon alijibu bila kuwa na wasiwasi:-
"Mimi ninatafuta imani madhubuti ambayo nitaitegemea kunipa utulivu."
Walikubaliana na msimamo wake Kibon. Ila alimuonya kuwa, Waislam hawaruhusiwi kumshawishi yeyote kwa ujanja. Tunawalingania wale wanaotaka kufahamum kusema:-
"Mimi nina uhuru wa kuchagua imani niipendayo, hakuna mtu awezaye kunizuia."
Adul alikubaliana naye kwa alicho kisema. Pamoja na hilo, hakuna kulazimishana katika dini. Hata hivyo Kibon hakuwa mbali na maswali. Aliuliza kuwa, kwa nini Waislam huwa wanawata wjibu
"Hilo jibu lake ni rahisi, ni sawa kama vile Wakristo wanapo wataka Wayahudi wamkubaki Yesu kuwa ni Masihi. Waislam nao huwataka Wakristo na Wayahudi na walimwengu wote kumkubali Muhammad(s.a.w) kuwa ni Mtume
Ustadhi alidakia huku akiwa amesimama akijiandaa kutoka nje kisha alisema:-
"Mtume Muhammad (s.a.w) amesema: Nifikishieni ujumbe wangu japo kwa aya moja."
Kibon alihoji kuwa, anayoyasema Adul ni ya kwenye Qur'an. Je, kwenye Biblia? Bila ya kuwa shaka, Adul alimpa jibu:-
"Isaya 21:31 ni ufunuo juu ya Arabuni. Ina maana kuwa, jukumu la kueneza Uislam litakuwa kwa Waarabu Waislam, na hasa kwa Waislam wote.
Isaya 21:7 inasema hivi, Naye akiona kundi là wapandanda farasi, wakienda wawili wawili na kundi la punda, na kundi la punda, na kundi la Ngamia asikilize sana, akajitahidi kusikiliza."
Kibon alikuwa bado hajaridhika. Ajuavyo yeye ni kwamba: Kundi la wapanda punda alikuwa Yesu wakati anaingia Yerusalemu. Yohana12:14 na Mathayo 21:5, sasa kundi la wapanda Ngamia ni nani? Adul alikuwa tayari kwa majibu, alisema:-
"Huyo sio mwingine bali ni Muhammad (s.a.w) aliyekuja karibu miaka mia sita baada ya Masihi."
Mazungumzo waliyasitisha kwa dakika kumi, ili mwenye haja yake aimalize, ajenge akiri na hoja yakini. Mara hii walipo kutana tena walianza mazungumzo. Naye Adul alianza kwa kusema:-
"Sasa jamani, tujadili tofauti zilizopo kwa uwazi bila chuji. Uislam umesimama juu ya misingi ya kiakili, sio ukubali tu. Soma Biblia Wathesalonike 5:21.
Kibon aliisoma kwa taratibu sana kuhakikisha kwamba haruki hata herufi moja. Alisoma hivi:-
"Wathesalonike 5:21 Inasema hivi, jaribuni (hakikisheni) mambo yote, lishikeni lililo jema."
Kibon alipomaliza kuisoma aya hiyo, alimuomba amrudishe nyuma. Alimuuliza iwapo Muhammad katabiriwa ndani ya Biblia na ni Agano lipi?
Adul alimjibu kuwa, Muhammad (s.a.w) katabiriwa katika maagano yote mawili, lakini hawezi kuamini ikiwa haamini umoja yaani upweke wa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo Kibon alidai kuwa bado hajamwelewa. Ndipo alipomfafanulia kuwa:-
"Nina maana kuwa, iwapo unaendelea kuamini utatu, Uungu wa Yesu, Yesu ni mtoto wa Mungu, Dhambi ya asili na kafara. Hizi ni imani au itikadi zilizo buniwa na watu tu. Kwa uthibitisho tusomee Mathayo 15:9."
Kibon alifunua kurasa za Biblia kuitafuta Mathayo 15:9 akaisoma hivi:
"Mathayo 15:9 inasema hivi, Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu."
Baada ya kusoma maandiko hayo, Adul alimwachia Ustadhi aendelee na mahojiano. Hapo hapo alitaka kujua iwapo Biblia ni neno takatifu. Lakini Kitin alijibu haraka haraka na kukubali kuwa, Biblia ni neno takatifu. Ndipo Ustadhi alipomwambia Kitin asome Luka 1:2-3. Aliisoma hivi:-
"Inasema: Kama walivyo tuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami kwa kiwa nimejitafutoa ushahidi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofili Mtukufu."
Ustadhi alimuuliza Kitin iwapo ameelewa. Alizidi kumwelewesha kuwa, Luka hakuwa shahidi wala hakuona, mafundisho aliyo yakusanya amehadithiwa na mashaidi waliyo yaona, na sio Ufunuo kutoka kwa Mungu. Alimuuliza iwapo sasa anaaminije kuwa Biblia ni neno la Mungu? Lakini Kitin alimjibu Ustadhi:-
"Huenda ni sehemu hii tu ndio sio neno la Mungu."
Ustadhi naye alimuuliza swali kuwa je, anaelewa kuwa Biblia imefanyiwa marekebisho mengi huko nyuma? Kitin alisema yeye hajui. Ustadhi aliendelea kumfahamisha:-
"Sasa nakufahamisha kuwa, The Revised Standard Version Bible y mwka 1952 na 1971, New American Standard Bible na New Translation of the Holy Scripture zimeondoa baadhi ya baya. Ukilinganisha na King James Version, Leader's Digest imeandika kuwa: Agano la Kale limenywea asilimia hamsini, na Agano Jipya limepungua asilimia ishirini na tano. Pia miaka ya karibuni wataalam wa Kikristo walitaka kufuta mistari inayoelezea matusi na mambo ya aibu katika Biblia. Je, ina maana Biblia Takatifu haina makosa?"
Kitin alijibu kwa ufupi sana kuwa, ndiyo inayokusudiwa, nae pia akamtupia swali, kwani yeye anakusudia makosa gani? Ustadhi alimpa jibu na swali:-
"Mokosa ninayo kusudia ni haya, je, fulani akitajwa kwenye aya mbili tofauti kuwa alikufa akiwa na umri tofauti. Habari hizo zinaweza kuwa sahihi?"
Kitin alikana kuwa, sahihi yaweza kuwa moja wapo tu. Ustadhi alimuuliza tena iwapo kitabu kitakatifu zimo aya zinazo pingana utasema ni kitabu kitakatifu? Kitin alikana tena kuwa, kitabu kitakatifu ni Ufunuo kutoka kwa Mungu, haiwezekani yawemo makosa au zenye kipingana.
Ustadhi alimuuliza kwa mara nyingine, iwapo kitabu kama hicho siyo kitakatifu. Nae Kitin aliikubali kuwa utukufu wa kitabu hicho utakuwa umepotea.
Ustadhi aliendelea kumuuliza Kitin iwapo ni mia kwa mia hakiamini kitabu, anafikiri ni kwa sababu gani inawezekana kuwepo kwa migongano kama hiyo.
Kitin alijibu kuwa huenda ni makosa yatokanayo na uandishi au mageuzi ya kusudi ya mwandishi, kwa kupunguza au kuzidisha.
Ustadhi alizidi kumpa maswali Katin, alimuuliza kuwa kama kuna aya zinazopingana ndani ya Biblia; je, bado anashikikilia kwamba Biblia ni takatifu? Lakini Katin bado alikuwa anakanusha kwmba hajawai kuona aya zinazo pingana.
Pamoja na kukanusha huko, alidai ni agano lipi lenye mgongano? Ndipo alipo fahamishwa kuwa ni maagano yote mawili. Alimtaka asome Biblia, Samweli wa Pili 8:4 na Mambo ya Nyakati wa Kwanza 18:4. A alisoma kwa sauti:-
"2Samweli 8:4 inasema hivi, Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na MIA SABA, na askari walio kwenda kwa miguu ishirini elfu.
"1 Mambo ya Nyakati 18:4 inasema, Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi SABA ELFU na askari waendao kwa miguu ishirini elfu."
Ustadhi alimuuliza Kitin kuwa ni lipi sahihi, mia saba au sabini elfu? Kipengele hiki alikosa jibu. Kisha aliombwa aendelee na Samweli wa Pili 10:18 na Mambo ya Nyakati wa Kwanza 19:18:-
"2Samweli 10:18 inasema hivi, wakakimbia Washami mbele ya Israeli; nae Daudi katika Washami WATU WA MAGARI MIA SABA na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo SOBAKI, jemedari wa jeshi lao, hata akafa huko.
"1Mambo ya Nyakati 19:18 inasema hivi, Washami wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua katika Washami WATU WA MAGARI SABA ELFU, na askari waendao kwa miguuu AROBAINI ELFU, na akamuua na SHOBAKI jemedari wa jeshi."
Je, Ustadhi alimuul Kitin, ni watu wa magari mia saba au saba elfu? Wapanda farasi ni arobaini elfu au ni askari waendao kwa miguu? Sobaki au Shobaki?.
Kulikuwa na minong'ono ya hapa na pale, kwani kilicho kuwa kinazungumziwa kiliwakuna vichwa. Ustadhi alimuomba Kitin aendelee na Wafalne wa pili 8:26 na Mambo ya Nyakati wa pili 22:2:-
"2Wafalme 8:26 inasema hivi, Ahazia alikuwa na umri wa miaka ISHIRINI NA MIWILI alipo anza kutawala."
"2Mambo ya Nyakati 22:2 inasema hivi, Ahazia alikuwa na umri wa miaka AROBAINI NA MIWILI alipo anza kutawala."
Ustadhi alihoji, je ni miaka ishirini au arobaini Ahazia alipo anza kutawala? Jibu lilionekana lakini ilikuwa ni kimya kimetanda, hakuna aliyejibu kwa sauti bali lilikuwa ni la kila mmoja rohoni mwake.
Kitin alionekana kuchoka, lakini Ustadhi alimhimiza aendelee kusoma Samweli wa Pili 23:8 na Mambo ya Nyakati wa kwanza11:11. Aliendelea kusoma:-
"2Samweli 23:8 inasema, Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi.Yashobeamu, Mhakmoni, mkuu wa maakida, huyo aliinua SHOKA lake juu ya WATU MIA NANE waliuawa pamoja na baada yake kulikuwa na Eleazari mwana wa Dadai, Mwahoni."
"1Mambo ya Nyakati 11:11 inasema hivi, Hii ndiyo hesabu ya hao mashujaa aliokuwa nao Daudi, Yashibeamu,Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo alinua MKUKI wake juu ya WATU MIA TATU akawaua pamoja."
Ustadhi alihoji. Je, ni shoka au mkuki? Watu mia nane au mia tatu? Alimtaka Kitin asome kwa mara nyingine Sanweli wa pili 24:1 na Mambo ya Nyakati wa Kwanza 21:1. Alisoma:-
"2Samweli 24:1 inasema hii, Tena hasira ya Bwana ikawa juu ya Israeli, akamtia Daudi nia juu yao, akisema, nenda, ukawahesabu Isreli na Yuda."
"1Mambo ya Nyakati inasema hivi, Tena shetani akasimama juu yao Israeli, akamshawishi Daudi akawahesabu Israeli."
Ustadhi alihoji kwa mara nyingine. Je, ni lipi sahihi, Daudi au Shetani? Hakuiishia hapo, alihimiza wendelee na Samweli wa Pili 6:23 na 21:8
Kitin alikuwa amechoka, na hasa akitafakari migongano anayoiona ndani ya Biblia, ilibidi amwambie Love aendelee kusoma maandiko. Bila kusita alianza kusoma:-
"2Samweli 6:23 inasema hivi, Basi Mikali binti wa Sauli, HAKUWA NA MTOTO hata siku ya kufa kwake."
"2Samweli 21:8 inasema hivi, Ila Mfalme akatwaa hao wana wawili wa Respa, binti Aya, aliomzalia Sauli, Armoni na Mefiboshethi na wana watano wa Merabuu binti Sauli, aliomzalia Adrieli, Mwana wa Barzila, Mmeholathi."
Ustadhi aliendelea na hoja. Aliuliza je, Mikali alikuwa na watoto au laa? Jina Mikali limo katika Version ya King James na New World Translation of the Holy Scripture inayotumiwa na Jehovah's Witnesses. Jina hilo limebadirishwa kuwa Merabu katika New American Standard Bible ya 1973. Pia Biblia ya Kiswahili Union Version ya 1952 lipo jina Merabu.
Love aliwauliza wenzake iwapo kuna zaidi ya hilo kwani alikuwa hajawahi kuiona migongano hiyo.
Ustadhi aliwauliza iwapo kama haitoshi kuukana utakatifu wa Biblia? Lakini aliona sio kitu aendelee kusoma Mwanzo 6:3, 9:29, 5:32, 7:6. Love alisoma:-
"Mwanzo 6:3 inasema hivi, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama, basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini."
"Mwanzo 9:29 inasema hivi, Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa."
"Mwanzo 5:32 inasema hivi, Nuhu alikuwa mwenye miaka miaka mia tano."
"Mwanzo inasema hivi, Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi."
Ustadhi na wote walikuwa na ukimya uliodumu yapata dakika mbili hivi, nadhani kila mmoja alikuwa anajaribu kuchambua hili na lile. Ndipo Ustadhi aliwauliza tofauti zilizomo kwenye Biblia wameziona? Wote kwa pamoja walimjibu kwamba wameziona.
Muda wa chakula cha mchana ulikuwa umetimia, waliondoka kila mmoja alikuwa anajinyoosha viungo vya miili yao, hii iliashiria kuwa ni uchovu wa kukaa muda mrefu pia msongo wa mawazo wa kutafakari hili na lile.
Sura ya "7"
Baada ya chakula cha mchana, walijumuika tena kuendelea na mazungumzo yao. Kila mmoja alikuwa ni mcheshi, wote waliyafurahia mazungumzo yao. Nae Kahin alifungua kikao kwa kusema:-
"Mjomba, sisi Wakristo, Mungu alimuuba mwanadamu kwa mfano wake. Nataka kuelewa huo mfano, mweupe, mweusi, mume au mke?
Adul alimwelewa vizuri sana Kahin. Alimtaka yeye mwenyewe awasomee mwanzo 1:26, Isaya 40:18 na 25 kisha Zaburi 89:6 na pia Yeremiah 10:6 na 7. Alianza kusoma:-
"Mwanzo 1:26 inasema hivi, Mungu akasema, na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu."
"Isaya 40:18 inasema hivi, Basi mtanilinganisha na Mungu nani? Au mtanifananisha na mfano wa namna? Mtanifananisha na nani basi nipate kuwa sawa nae? Asema yeye aliye mtakatifu."
Maana ni nani katika Mbingu awezaye kulinganishwa na Bwana? Ni nani afanane na Bwana...?"
"Yeremiah 29:6 na 7 inasema hivi, Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Eee Bwana..... Hapana hata mmoja kama wewe.
Adul alimuuliza Kahin, iwapo ameyaona hayo. Alikubali kuwa ameyaona. Lakini alimwambia kuwa hayo yamo kwenye Agano la Kale. Bila kupoteza muda. Adul alimtaka asome Agano jipya, afungue Yohana 5:37 na 14:9, 5:31 na 8:14. Nae alisoma:-
"Yohana 5:37 inasema hivi, Mimi nikijishuhudia mwenyewe ushuhuda wangu si kweli."
"Yohana 14:9 inasema hivi, Yesu akajibu akamwambia, mimi ingawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda ni kweli."
"Yohana 5:31 inasema hivi, Sauti yake hamkuisikia wowote, wala sura yake hamkuiona."
"Yohana 8:14 inasema hivi, Aliye niona mimi amemuona Baba." Adul aliwaambia kuwa hiyo ni mifano miwili inayo pingana katika Agano Jipya. Lakini ipo chungu nzima kama wataendelea kujadiliana juu ya imani za Ukristo kama vile Imani ya Utatu, Uungu wa Yesu, Yesu mtoto wa Yesu, Dhambi ya asili na kafara. Kuvunjiwa heshima Mitume mbalimbali kwa kuzuliwa wanaabudu miungu ya uongo na kushutumiwa vitendo na maharimu wao, kuwanajisi wanawake kwa nguvu na vitendo vingine vya zinaa.
Lakini Kahin hayakumwingia akilini bado alikuwa na mashaka ndani yake. Alihoji kuwa, hayo yote yapo wapi ndani ya Biblia? Papo hapo alitakiwa asome Mwanzo 9:23-24, Wafalme wa kwanza 11:9-10 kutoka 32:4, Mwanzo 19:36, Mwanzo 29:28, Samweli wa Pili 11:4-5, Kumbukumbu la Taurati 23:2, Samweli wa Pili 16:22 na Mwanzo 38:18: alianza kusoma:-
"Mwanzo 9:23-24 inasomeka hivi, Shemu na Yafethi wakatwaa vazi wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyume nyume, wakamfunika uchi wa baba yao, na nyuso zao zilielekea nyuma wala hakuona uchi wa baba yao. Nuhu akaelevuka katika ulevi wake akajua mwana wake mdogo aliyemtenda."
"1Wafalme 11:9-10 inasema hivi, Basi mwana akamghadhabikia Suleiman....akamwamuru katika habari ya jambo hilo hilo asifuate Miuungu mingine, lakini yeye hakuyasikia aliyoyaamuru Bwana."
"Kutoka 32:4 inasema hivi, Harun akapokea hereni za dhahabu mikononi mwao. Akazitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha, nao wakasema, hiyo ndiyo miuungu yako, Ee Isreali iliyokutoa katika nchi ya Misri.
" Mwanzo 19:36 inasema hivi, Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao."
"Mwanzo 29:28 inasema hivi, Yakobo akafanya hili, akatimiza siku zake saba. Naye Labani akampa Raheli binti yake kuwa mkewe."
"2Samweli 11:4-5 inasema hivi, Basi Daudi akapeleka wajumbe, akatwaa mke wa Uria, nae akaingia kwake, naye akalala nae, maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake, kisha akarudi nyumbani kwake. Yule mwanamke akachukua mimba, basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, ni mja mzito."
"Kumbukumbu la Taurati 23:2 inasema hivi, Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana."
"Samweli 16:22 inasema hivi, Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini, naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote.
" Mwanzo 38:18 inasema hivi, Basi akampa pete, kamba na fimbo yake, akaingia kwake, naye akapata mimba."
Adul alifafanua kwa ufupi maandiko hayo kwamba. Nuhu amezuliwa, kwamba alilewa na kukaa uchi mbele ya watoto wake baleghe.
Suleiman naye kazuliwa kuabudu miungu ya uongo.
Haruni pia amezuliwa kuwa alichonga sanamu ya ndama wa dhahabu, ili wana wa Israeli waiabudu.
Nuhu Lutu wamesingiziwa kufanya vitendo vichafu na binti zake wawili.
Yakobo amesingiziwa alioa ndugu wawili wakati ni mmoja.
Daudi naye inaoneshwa kuwa alizini, kama ndivyo vipi Daudi akubaliwe kuwemo katika nasabu ya Yesu ikiwa imeanzia na mtu aliye zini.
Absalomu kazuliwa kufanya zinaa na masuria wa baba yake Nabii Daudi.
Yuda nae kasingiziwa kufanya uovu kwa mkewe Tamari. Ingawa Mayahudi na Waislam ni madui wakubwa. Muislam hathubutu kuandika kitabu akamsingizia Mtume yeyote wa Kiisreaeli kama vile Yuda, Daudi, Yesu na wengineo wenye mambo maovu kama hayo.
Unadhani Mwenyezi Mungu aliwaleta Mitume wasiofaa kuja kuongoza wenzao? Hii siyo kweli.
Kahin naye alisema kuwa hayo hayafikirii hivyo. Ila aliuliza swali kuwa, kwani yeye Adul haiamini Biblia? Jibu alipewa kuwa:-
"Waislam tunaamini vitabu vyote vilivyo teremshwa vikiwa katika asili yake. Kila Mtume aliletwa katika kila umma ili awe muonyaji. Vitabu viliteremshwa kwa baadhi ya Mitume ili ni miongozo kwao.
"Nabii Musa alikuwa na Taurati, Nabii Ibrahim aliku na Sahuf, Nabii Daudu alikuwa na Zaburi, Injili ni kwa Yesu. (Nabii Issa a.s), na mwisho Mtume Muhammad akiwa na Qur'an ili iwe muongozo kwa wanadamu wote, popote na wakati wowote. Hata hivyo Yesu mwenyewe alikuja kwa watu wa Israeli tu.
"Ushahidi ni Mathayo 15:;24 ambayo inasema kuwa: Sikutumwa ila kwa Kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli."
"Pia Mathayo 1:21 inasema, Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina Yesu, maana, yeye ndiye atakae waokoa watu wake na dhambi zao."
Kahin alitulia kidogo huku akitafakari alipo ulizwa kuhusu maandiko hayo anasemaje? Baadae alisema kuwa, hana ubishi, lakini mbona katika Marko 16:15 inasema hivi:-
"Akamwambia, enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injli kwa kila kiumbe.
Adul alimwelewesha Kahin kuwa, hayo anayo yasoma yamepingana na Mathayo 15:24 na 1:21. Halafu Marko 16:9-20 imeondolewa kwenye Biblia nyingi. Biblia ya The New American Standard, sehemu hiyo wameiweka kwenye mabano na kutoa maelezo yafuatayo:-
" Baadhi ya nyaraka za kale hazina aya 9 mpaka ya 20."
Adul alijiweka sawa huku akiiweka sawa miwani yake kisha aliendelea kumuelewesha Kahin:-
"Ukweli huo umo hata kwenye kitabu cha The New World Translation of the Holy Scriptures, pia Revised Standard Version,chini ya aya hizo kuna maneno yasemayo kuwa: Baadhi ya nyaraka za kale zimeishia katika aya ya 8..... Hii ina maana, hata kufufuka kwa Yesu sio kweli, sababu habari hii imo katika Marko 16:9."
Kahin alikuwa bado hajaridhika na maelezo aliyopewa, alizidi naye kutoa hoja ndai ya aya, akasema:-
"Mbona Mathayo 28:19 Yesu amesema: Basi, enedeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi."
Adul hakuchelea aliendelea kumpa somo ndugu yake Ila. Alimweleza kuwa:-
"Sawa, The New American Standard Bible na New World Translation Scriptures haikutafasiri Mataifa yote yaani 'All Nation', isipokuwa imetafasiri 'Yale Mataifa yote kwa maana'all the nations. Hapa inakusudiwa ni yale makabila kumi na mbili ya Israeli."
Adul aliitoa miwani yake machoni, akawa anaisafisha kwa kitambaa chake, huku akimkazia macho Kahin kisha alimuuliza:-
"Kahin, fikra yako ni nini juu ya Biblia?
Swali hilo kwake halikuwa zito kulijibu kwani alikuwa tayari kisha iona njia ya kupita. Moja kwa moja alijibu:-
"Ukweli kwa sasa Biblia imeanza kutetereka. Pia Imani yangu itafumbuliwa na Uislam hasa tutakapofikia kujadili tofauti zetu."
Sura ya "8"
Baada ya mapumziko mafupi walirejea kwenye mazungumzo yao. Safari hii walianza na mjadala wa Imani ya utatuj. Yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu. Ustadhi aliwauliza wapwa zake iwapo bado wana Imani ya Utatu. Kibon alitoa jibu:-
"Kwangu mimi bado nina Imani, kwani Mathayo 5:7 na 8 inasema, Naye roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao Mbiguni, Baba, na neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni mmoja."
Ustadhi alikanusha maandiko hayo, aliwafahamisha kuwa, Utatu huo haumo kwenye mafunzo ya Biblia; wala neno Utatu halimo kamwe ndani ya Biblia, tena katika Kamusi za Biblia haukutajwa, hata Yesu mwenyewe hakufundisha. Hivyo basi hakuna ushahidi unaokubalika ndani ya Biblia.
Kibon aliuliza kuwa inakuwaje hayo ya Mungu Baba na kadhalika yatajwe kwenye Biblia? Naye Usitadhi alitoa uwelewesho kwamba:-
"Sikiliza, hayo yamo katika King James Version ya mwaka 1611 na ndiyo ushahidi wabImani ya Utatu, lakini kipande hicho kimeondolewa katika Revised Standard Version ya 1952 na 1971 na Biblia nyingine nyingi, sababu ilikuwa ni kosa lililojitokeza katika Biblia ya Kiyunani."
" Biblia ya The New American Standard Bible, waraka wa kwanza wa Yohana 5:7 na 8 inasema: ' Naye Roho ndiye ashudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washudiao, Roho, maji, na damu na watatu hawa ni mmoja."
Baada ya ufafanuzi huo Ustadhi aliwauliza kuwa hivi wao hawajui kama sehemu hizo zimeindolewa? Hata mapadri na wahubiri hawayajui hayo.
Bado Kibon alitoa hoja ya kwamba, mbona Mathayo 28:19 inatosha kuwa ushahidi wa utatu kwani bado inasema kuwa:-
"Mkiwabatiza kwa jna la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu."
Ustadhi alifanya juhudi kubwa sana kumfahamisha mpwa wake pamoja na wengine, kwa kusema:-
"Imani hii imekuzwa na upagani wa Kirumi kwamba ni Mungu mmoja mwenye imani tatu. Sabato imegeuzwa kuwa Jumapili, tarehe 25 Desemba ni siku ya kuzaliwa Yesu badala ya Mitthra Mungu Jua. Kupamba miti ya Krismas Biblia imekataza ingawa bado mnayafuata."
Kibon alikuwa mwepesi wa kushika, kuchambua na kutoa hoja. Aliuuliza kuwa hayo ya mti wa Mkrismas wapi yalipo kwenye Biblia? Ustadhi alimwambia asome Yeremiah 10:2-5 inasemaje. Naye aliisoma hivi:-
"Bwana asema hivi, msijifunze njia ya Mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara hizo. Maana desturi za watu hao ni batili, maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazu ya mkono ya ufundi na shoka. Hupamba kwa fedha na dhahabu, huukaza kwa msumari na nyundo, usitikisike. Mfumo wao ni mfano wa Mtende, kazi ya cherehani, hawasemi, hawana budi kuchukuliwa kwa sababu hawezi kwenda. Usiwaogope, kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema." Kibon alikuwa bado yumo katika muhangaiko wa kuyatafakari aliyo yapata, kwani bado alikuwa na la kuuliza. Aliuliza:-
"Mjomba, hivi maelezo hayo unakusudia kutuambia nini?
Ustadhi aliendelea kumuweka sawa mpwa wake Kibon alimfafanulia kwa makini kwamba:-
"Nia yangu mimi mjomba, ni kukufahamisha kuwa, Ukristo umeyaacha mafundisho ya asili ya Yesu. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.) akamleta Mtume Muhammad (s.a.w.) kuja kuhurisha na kurejesha imani sahihi zilizo potoshwa kama vile: Kalenda ya Kirumi 'Roman Julian Calendar' imefanywa ndiyo Kalenda ya Kristo, Nguruwe hakuharamishwa, kutahiri kulikatazwa na Paulo. Katika Wagalatia 6:2."
"Wagalatia hiyo inasema: Tazama, mimi Paulo nawaambia nyinyi kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno."
Palikuwa na ukimya ni ukimya wa kheri tu. Walitazamana kwa tabasamu za upendo. Mara Kibon aliibuka na hoja hiyo hiyo ya Imani ya Utatu. Qur'an inasemaje. Ustadhil alimuomba Kulut asome Qur'an ura ya 5:73:-
"Qur'an 5:73 inasema hivi, Kwa hakika wamekufuru wale walio sema, Mwenyezi Mungu ni mmoja katika wale waungu watatu. Hali hakuna Mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja (tu peke yake). Na kama hawataacha hayo wayasemayo, kwa yakini itawakamata wale wanao endelea na ikafiri miongoni mwa adhabu iumizayo."
Ustadhi aliwauliza iwapo bado wanaikubalia Imani ya Utatu ambayo Yesu hakuifundisha. Mara ghafla Love aliibuka. Alikuwa anafuta futa nguo yake iliyo angukiwa na uchafu toka darini. Kisha alisema:-
"Hata hivyo Mungu na Yesu ni mmoja kama tunavyo soma Yohana 14:11; isemayo, 'Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu."
Ustadhi alitabasamu, akamwangalia Love kisha kwa sauti ya chini alimwambia awasomee Yohana 17:21: Love aliisoma:-
"Yohana 17:21 inasema hivi, Wanafunzi wote wawe na umoja, kama wewe, baba ulivyo ndani yangu, ndani yako, hao nao wawe ndani yetu."
Ustadhi kama kawaida yake hakuishia kutabasamu, kwa sauti ya upole aliendelea kuwauliza, kwa nini wanafunzi hawakuitwa Mungu au Miungu? Hapo hapakuwa na jibu.
Palikuwa kimya, hakuna aliweza kutoa jibu, walibaki wanatazamana mmoja baada ya mwingine. Ndipo Usitadhi akasema:-
"Hili lipo wazi kuwa Mungu na Yesu ni moja, lakini vile vile wanafunzi nao ni wamoja katika Yesu na Mungu. Kwa sababu Yesu yu ndani ya Mungu. Hivyo wanafunzi nao kwa nini wasiwe waungu kama vile Yesu kwa kuwa nao wako ndani ya Mungu?"
Walioelewa walielewa kila mmoja alikuwa na upeo wake wakuelewa. Ustadhi alizidi kutoa maelezo:-
"Ikiwa Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu wanakuwa ni Mungu wa nafsi tatu, tukiwajumlisha na wanafunzi watakuwa ni Miungu wa nafsi kumi na tano." Love alikuwa bado na msimamo wake, aliendelea na machachali yake ya kutaka kuelewa. Alisema:-
"Yohana 14:9 inasema hivi, Aliyeniona mimi amemwona Baba." "Ndiyo kusema Yesu ni Mungu."
Ustadhi alitabasamu kisha alimnyoshea ki Love akamwambia asome Yohana 14:8 na 14:9. Aliisoma hivi:-
"Yohana 14:8 insema hivi, Filipo akamwambia Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha."
Yohana 14:9 inasema hivi, Yesu akamwambia , mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usimjue, Fulipo? Aliyniona mimi , amemuona Baba, basi wewe wasemaje, utuoneshe Baba?"
Ustadhi alianza tena kazi ya kuwaelewesha wapwa zake kwa kusema hivi:-
"Hao ina maana, Yesu akamwambia Filipo, vipi nikuonyesheni Mungu jambo ambalo haliwezekani? Mwamini Mungu, kuzingatia alivyoviumba, jua, mwezi na chochote alicho kiumba pia Yesu mwenyewe aliyeumbwa na Mungu."
"Kwa ufupi Yohana 4:21 inasema hivi, Mungu ni Roho. Hiyo hiyo Yohana 5:37 inasema hivi, Sauti yaje hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona. Sasa nawauliza kuwa utawezaje kuiona Roho?"
Wote walikuwa wameinamisha vichwa vyao, kwa pamoja walijibu kuwa, hakuna. Ismail akiwaeleza kuwa, kama hakuna awezaye kuiona Roho, ndiyo kusema walimuona Yesu na wala sio Mungu. Hata hivyo Paulo naye katika Timotheo 6:16 anasema, Wala hakuna mwanadamu aliyemuona wala awezaye kumuona.
Naye Love alimtaka mjomba wake Ismail awaeleweshe ndani ya Qur'an inasema nini. Ustadhi aliisoma hivi:-
"Qur'an 6:103 inasema hivi, Macho hayamfikii kumona, bali yeye anayafikia macho kuyaona na kuwaona hao wenye macho. Naye ni mwenye kujua yaliyo fichikana na yaliyo dhahiri."
Kibon aliyekuwa anapiga miayo na kukohoa kama mtu aliyepariwa, alimwita mjobaye na kusema:-
"Mjomba, ukweli ni kwamba ni taabu sana sisi kukataa tuliyo fundishwa tangu utotoni mwetu."
Ustadhi alizidi kuwaambia kuwa, yatakayo fuata anadhani yatawapa mwangaza zaidi kuhusu Utatu, hasa Roho Mtakatifu ni nani. Hapo hapo Kibon alisema:-
"Roho Mtakatifu ni Mungu pia, Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu. Haturuhusiwi kusema wauungu ni watatu, ila Mungu ni mmoja tu."
Ustadhi alimwambia Kibon kuwa asiwe na haraka bali waende taratibu. Alimwambia asome Mathayo 1:18 na Kuka 1:26-27. Kibonalianza kusoma:-
"Mathayo 1:18 inasema, Kuzaliwa kwake Kristo kulikuwa hivi, Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
"Luka 1:26-27 inasema hivi, Mwezi wa sita, Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu,wa mbali na Daudi, na jina lake bikira huyo ni Mariamu."
Ustadhi alimwangalia Adul, kisha akawaangalia wao na wenzake, akawauliza iwapo wameona jinsi Yesu kuzaliwa kwake kimiujiza. Roho Mtakatifu katajwa na Mathayo, Malaika Gabrieli katajwa na Luka. Sasa Roho Mtakatifu ni nani basi? Kibon alitoa jibu:-
"Mjomba, Roho Mtkatifu ni Malaika Gabrieli."
Ustadhi aliendelea kuwauliza wengine iwapo bado wanaikubali Imani ya Utatu. Lakini wote walikuwa kimya, wakitegeana nani ajibu. Ndipo Love aliposema kuwa, basi ina maana Mungu ni Mungu, Roho Mtakatifu ni Malaika Gabrieli, lakini alishindwa kumalizia kuwa Yesu ni nani. Ila Ustadhi alimsaidia kwamba:-
"Yesu ni Mtume, mwana wa Mariam."
Kibon alionoekana kusema kitu, lakini alishikwa na kigugumizi, ilibidi atulie kwanza kwa muda ndipo alipo mwambia kuwa atalitatua vipi kile wanachokiita fumbo?wa ufupi alimwelewsha kuwa Qur'an ni kigezi cha masahihisho cha kuona mabadiliko ndani ya vitabu vilivyo teremshwa kabla.
Baada ya maelezo hayo Ustadhi aliwauliza iwapo sasa wanaamini kiwa Mjomba ni mmoja?, Yesu ni mwana wa Mariam na ni Mtume? Wote kwa pamoja kwa sauti zenye furaha waliiitikia:-
"Tunaamini mjoba, mjomba tunaamini, tuanaami kabisa kabisa Mungu ni mmoja tu. Vile vile tunakubali kuwa Yesu ni mwana wa Mariam na ni Mtume."
Ustadhi alijitengeneza, alijigeuza geuza , akapumua kwa nguvu, akawatupia macho, kisha akawauliza:-
"Kama mnaamini hivyo, kwa sababu gani hamrudi hatua moja zaidi na kumkubali Muhammad kuwa ni Mtume wa mwisho? Wale mnao mkubali Muhammad kwa hiyari yao, nifuatisheni matamshi nitakayo yatamka.
"Nina kubali kuwa hapana Mungu ila Allah, asiye na mshirika, na Muhammad ni mtumishi na Mtume wake. Ash hadu an ka llah Illah lahu Wadahu la Sharikalah Wa ash hadu anna Muhammadn Abduhu wa Rasuluhu."
Walisikiliza kwa makini matamshi yaliyo tamkwa na Ustadhi, baada ya hapo Kibon aliuliza kuhusu ndugu zake huko waliko lelewa, kwamba wao ni Wakristo na anapenda kuishi nao. Je, itakuwaje? Ustadhi alimwambia, mtoa jibu ni Qur'an. Alimtaka asikilize inasema nini Qur'an 17:15:-
"Qur'an 17:15 inasema hivi, Anaeongoka, basi anaongoka kwa maslahi yake mwenyewe, na anaepotea, basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake mwenyewe. Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine. Na sisi si wenye kuwadhibisha viumbe mpaka tuwapelekee Mtume awafundishe yaliyo ya haki. Basi wanapo yakataa ndipo wanapo adhibiwa."
Kibon alikiri kuwa amemuelewa mjomba wake Ustadhi, pamoja na wengine nao walikiri kuwa wamemuelewa. Lakini Kitin alitaka kujua iwapo inawezekana kufuata dini zote mbili. Ustadhi alifungua kitabu cha Qur'an akamwambia Kitin asikilze:-
"Qur'an 4:150-152 inasema hivi, Hakika wanao mkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume yake na wanataka kutenga baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume yake kwa kusema: Wengine tunawamini na wengine tunawakataa, na wanataka kushika njia iliyo katikakati ya haya si ya Kiislamu khasa, hao ndio makafiri kweli. Tumewaandalia adhabu idhalilishayo. Na walio mwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake wala wasimfananishe yeyote katika wao bali wamemwamini wote, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu."
Ustadhi aliwataka wapumzike na wasubiri chakula cha usiku, na Mwenyezi Mungu awajalie waweze kukaa tena siku iliyofuata.
Sura ya "9"
Siku iliyofuata walikaa tena kuendelea na mazungumzo yao. Kibon alitoa wazo kwa mjomba wake Ustadhi kwamba, wasitamke shahadah wasije wakajifunga kwenye ahadi hiyo. Ustadhi aliendelea kumuelewesha kuwa:-
"Mwenyezi Mungu (s.w.) hakuumba ulimwengu huu bure tu. Amekupa uwezo wa kutofautisha baina ya haki na batili. Amewaleta Mitume wengi wawe waonyaji. Sisi tumeumbwa ili tumwabudu yeye na tushindane katika kutenda kheri hapa duniani. Hivyo akili yako inakuwa timamu mara unapo bareghe, unakuwa umeisha fikia ahadi ya kutenda au laa. Zaidi ili muelewe, Kulthumu atusimee Qur'an 3:191 na sura ya 90:8-10, sura 51:56 na sura 18:7:-
"Qur'an 3:191 inasema hivi, .....Mola wetu hakuviumba hivi bure. Utkufu ni wako.......
"Nayo sura ya 90:8-10 inasema hivi, Je hukutupa macho mawili? Ulimi na Midomo miwili? Na tukambainishia zote njia mbili iliyo njema na iliyo mbaya?
Pia sura ya 51:56 inasema hivi, Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu,
Sura ya 18:7.inasema hivi, Kwa hakika tumevifanya vilivoko juu ya ardhi viwe pambo lake, ili kuwatazama ni nanikatika wao viumbe wenye vitendo vizuri zaidi."
Baada ya Ustadhi kutoa maelezo ndani ya Qur'an bado kulikuwa na mengi ya kuhojiana. Ustadhi Aliwauliza iwapo Yesu ni Mungu. Kahin alidakia hoja hiyo na kusema kuwa:-
"Kwa mujibu wa Biblia Injili ya Yohana1:1 inasema hivi, Hapo mwanzo kulikuwa na Neno, Naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." Ustadhi aliwakumbusha wapwa zake kwamba walikubaliana , kitabu kitakatifu ni lazima kiwe hakipingani Kahin alikubaliana nae lakini bado alikuwa anasisitiza kuwa Yesu ni Mungu.
Ustadhi hakuchoka kuwaweka sawa, alifungua Biblia na kusoma kimoyo moyo, kisha akamwambia Kahin asome Kumbukumbu 6:4, Isaya 44:6, na 45:18 Isaya:-
"Kumbukumbu 6:4 inasema hivi, Ee Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja."
"Isaya 44:6 inasema hivi, Bwana ....asema hivi Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mini hapana Mungu."
"Isaya 45:18 inasema hivi, Maana Bwana , aliziumba Mbigu asema hivi, yeye ni Mungu ndiye aliyeifanya imara, hakuiumba ukiwa, aliumba ili ikaliwe na watu, Mimi ni Bwana wala hapana mwingine."
Ustadhi alianza kuyafafanua maandiko hayo kila mmoja akimsikiliza kwa makini zaidi. Alisema kuwa, Isaya 45:18 inathahakijishia kuwa Mungu peke yake ndiye, muumbaji na si mwingine yeyote, hata Yesu hakushiriki katika uumbaji.
Aliwarejesha kwenye Kumbukmbu 4:45, Kutoka 8:10, 2Samweli 17:22, 1Wafalme 8:23, 1Mambo ya Nyakati 17:20, Zaburi 86:8, 89:6 na 113:5, Hosea 13:4 na Zaburi 14:9. Lakini Kahin alikuwa tofauti na Ustadhi kwa kusema:-
"Mjomba mbona hayo yote yamo kwenye Agano la Kale, je, Agbano Jipya?"
Ustadhi aliendelea kufungua kurasa za Biblia taratibu bila kuwa na shaka yoyote, kisha alisema kuwa asipate shida, asome Marko 12:29, 1.Wakorintho 8:4 na 1.Timotheo 2:5. Kahin alianza kusoma:-
"Marko 12:29 inasema hivi, Yesu akanijibu, ya kwanza ndiyo hii, sikia, Israeli Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja."
"1.Wakorintho 8:4 inasema hivi, .....twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu."
1.Timotheo 2:5 unasema hivi, kwa sababu Mungu ni mmoja, na wapatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, mwanadamu Yesu Kristo."
Ustadhi aliwaambia maandiko yamesema nini katika Marko, Wakorintho, na Timotheo. Pia Yohana 1:1 je, si sawa na aya nyingine zilizo na makosa au kinyume chake?" Hakuna aliyetoa jibu mbali na Kibon alisema kuwa mambo ni magumu mno.
Ustadhi akawaambia kuwa waangalie ndani ya Qor,an 3:39 na 3:45 waone jinsi inavyo kubaliana na alivyosema Yesu ndani ya Biblia:-
Qur'an 3:39 inasema hivi, Mara Malaika wakamlingania, hali amesimama akisali chumbani, kwamba Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za kuwa utazaa mtoto, umwite Yahaya ambaye ni Yohana mbatizaji, atakaye kuwa mwenye kumsadikisha Mtume atakayezaliwa kwa neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu naye ni Nabii Issa na atakae kuwa Bwana kabisa na mtawa na Nabii anayetokana na watu wema."
"Qur'an 3:45 Hali kadhalika nayo inasema, Mungu anakupa habari njema za neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi, Isa, mwana wa Marian, mwenye heshima katika dunia na akhera, na miongoni mwa waliopelekwa mbele ya Mwenyezi Mungu."
Ustadhi alikuwa anawangalia wapwa zake jinsi walivyokuwa wanahangaika kunong'onezana ndipo alipowaambia kuwa, waangalie 1.Wakorintho 3:23 ambayo ilisomeka hivi:-
"Nanyi ni Wakristo, na Kristo ni wa Mungu."
Aliendelea kudadafua zaidi kwamba kwamba, basi Yohana 1:1 ilikuwa iandikwe hivi:-
".......na Neno lilikuwa la Mungu."
Aliendelea kuelezea kwamba yawezekana walikosea katika kutafasiri kutoka Kiebrania kwenda Kiyunani, ama yalifanyika makusudi. Kwani neno 'Theos' ni Mungu Kiyunani, lakini 'Theou' ni ya au la Mungu.
Alizidi kuwaelewesha kuwa, katika kamusi ya Kiyunani au Biblia ya Kiyunani au kitabu cha Prof. abdul Ahad Dawud, aliyekuwa Askofu wa Uramah kiitwacho 'Muhammad in the Bible uk.16. Utaona tofauti neno moja athari yake ni kubwa.
aliwahoji kwa nini Yesu ameitwa Neno la Mungu katika vitabu vyote viwili? Hapo hakuna alithubutu kujibu. Hapo ndipo alipo waambia kuwa jibu fupi ni Qur'an 3:47 isemayyo hivi:-
"Mariam akasema, Mola wangu nitapata mtoto na hali mtu yeyote hakunigusa? Akasema Mola wake, divyo vivyo, Mwenezi Mungu huumba anavyopenda, anapohukumu jambo huliambia, 'kuwa', basi likawa."
Kahin aliyekuwa amekaa kimya mwa muda mrefu alikuwa bado amejawa na hoja. Alisema:-
"Yesu alijawa na Roho Mtakatifu, hivyo ni Mungu."
Ustadhi, hakuona uzito wala usumbufu, alifungua Biblia akawa anaangalia ukurasa mmoja baada ya mwingine. Kisha akatulia, akamwauru Kahin awasomee Matendo ya Mitume 11:24:-
"Matendo ya Mitume 11:24 inasema hivi, Maana Barnaba alikuwa mtumwema amejaa Roho Mtakatifu na amani, watu wengi wakaongezeka upandenwa Bwana."
Ustadhi aliwaambia, kwamba wanaona jinsi huyo Barnaba alivyo jaa Roho Mtakatifu mbona hakuwa Mungu?"
Hapo palikuwa na ukimya, kila mmoja alikuwa ameangukia kufunua na kusoma kitabu alicho kuwa nacho mkononi. Ustadhi alizidi kumwambia Kahin aendelee kusoma Matendo ya Mitume 5:32:-
"Matendo ya Mitume 5:32 inasema hivi, Na sisi tu mashahidi wa mambo haya pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiie."
Ustadhi alizidi kuwapa elimu, aliwaambia kuwa Mungu ni Mungu pekee. Wataelelewa zaidi iwapo watasoma Matendo 6:5, 2.Petro 1:21, 1.Timotheo 1:14, Luka 1:41 na 1.Wakoritho 2:16.
Pamoja na ufafanuzi huo lakini bado Kahin alikuwa mgumu wa kuelewa alidakia na kusema:-
"Lakini Yesu alijawa na Roho Mtakatifu wakati bado yumo tumboni mwa mama yake."
Ustadhi alimjibu kuwa, hivyo ndivyo hata kwa Yohana Mbatizaji iliyokea. Alimwambia Kahin asome Luka 1:13, 15:-
"Luka 1:13, na 15 inasema hivi, Lakini yule MalaiKa akamwambia, usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa na mkeo Elizabethi atakuzalia mtoto mwanaume na jina lake utamwita Yohana......kwa sababu atakuwa Mkuu mbele za Bwana, hatakunywa divai wala kileo , naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye."
Kahin alionekana kuifahamu sana Biblia na siyo yeye tu hata wenzake, ndiyo maana alikuwa ni mwenye hoja za hapo na hapo. Bila kuchelelea lisema kuwa, Yesu alifanya Miujiza. Aliwalisha watu elfu tano kwa mikate mitatu na samaki wawili. Ustadhi alimjibu kuwa:-
"Kama ni miujiza, hata Elisha na Eliya walifanya. 2Wafalme 4:44 inasema hivi, Basi akawaandikia, nao wakala, wakasaza, sawa sawa na neno la Bwana."
"Katika 2Wafalme 4:7 inasema hivi, Enenda ukayauze mafuta haya, ulipe deni yako, nayo yàliyosalia uyatumie wewe na watoto wako."
"1Wafalme 17:16 inasema hivi, lile pipa la unga halikupunguka , wala ile chupa y mafuta haikuisha, sawa sawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya."
"1Wafalme 17:6 nayo inasema, kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa na maji ya kile kijito."
Ustadhi akimalizia kwa kusema kuwa, kama ni miujiza hata wengine waliifanya. Lakini Kahin alizidi kutoa hoja zake huku akimkazia macho Ustadhi. Akisema hivi:-
"Mjomba, Yesu aliweza kuponya ukoma."
Ustadhi alizidi kumwambia Kahin kuwa asome 2Wafalme 5:14 na 13:21. Kwani wapo wengine walio ponya.
"2Wafalme 5:14 inasema hivi, Ndipo akashuka akajichvya mara saba katika Yordan sawa sawa na neno lake yulemtu wa Mungu, nayo nyama ya mwili wake ikarudi kama nyama ya ya mtoto mchanga, akawa safi."
"2Wafalme 13:21 inasema hivi, ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi, wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha, mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka akasimama kwa miguu."
Mjadala mzima uliingiwa na kicheko kilichodumu zaidi dakika tano. Ndipo Nebort alipopata hoja nyingine kwamba:-
"Mjoba, lakini Yesu alitembea juu ya maji. Pia alitoa Mapepo."
Ustadhi alimwambia Kahin asome Kutoka 14:22, Mathayo 12:27 na 7:22, Luka 11:19:-
"Kutoka 14:22 inasema hivi, Wana wa Israeli wakaenda ndani katikati ya bahari katika nchi kavu, nayo maji yalikuwa ukuta kwa mkono wa kuume na wa kushoto."
"Mathayo 12:27 na Luka 11:19 zinasema hivi, Mimi nikitoa pepo kwa Beeleebul, je wana wenu huwatoa wa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakao wahukumu."
"Mathayo 7:22 inasema hivi, Wengi watniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako,bna kwa jina lako hatukutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?"
"Mathayo 24:24 inasema hivi, Kwa maana watatokea makristo wa ungo, na manabii wa uongo, na watatpa ishra kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule."
Ustadhi aliwafafanulia na hasa Kahin. Alimjuza kuwa hata Nabii Musa alinyoosha mkono wake juu ya bahari ikajitenga.
Utoaji wa mapepo ni kama ilivyo someka Mathayo 7:22 hii ilikuwa Yesu anawaasa wanafunzi wake.
Hali kadhalika Mathayo 24:24, huu ulikuwa ni ubashiri wa Yesu wa kutokea Manabii wa uongo.
Lakini bado Nebort alikuwa na msisitizo wake, aliendelea na hoja kama vile:-
"Miujiza iliyofanywa na Elisha na Eliya walifanya kwa kumuomba Bwana."
Hata Yesu naye alimuomba Bwana. Hili lilikuwa ni jibu la Ismail kutokana na Yohana 5:30 na Luka 11:20 zisemazo:-
"Yohana 5:30 inasema hivi, Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.
" Luka 11:20 inasema hivi, Lakini mimi nikitoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia."
Baada ya maelezo hayo, kulikuwa na kicheko cha hapa na pale. Kikiashiria kuwa mambo yatakuwa yale yale ya hoja za papo kwa papo za kijana Kahin.
Hata hivyo kabla Kahin hajaweka hoja zake Ustadhi aliendelea kusema kuwa miujiza yote aliyoifanya Yesu, pia Mitume wengine kabla yake waliifanya. Hata hivyo Yesu hakufanya miujiza mahali penye ukafiri. Kama watasoma Marko 6:5, 6 wataona inasema nini.
Kahin kama kawaida yake mwishoe wenzake walimwita jina la utani 'papo kwa papo'. Vicheko vilitawala mazungumzo. Walitulia baada ya dakika moja hivi kupita. Kahin aliendelea kusema kuwa:-
"Mjomba, lakini Yesu alifufuka siku ya tatu baada ya kufa."
Ustadhi alisema kwa ufupi kuwa, analolisK ni Injili ya Paulo, ambaye hakumuona Yesu katika uhai wake. Aliwaambia wasome 2Wafalme 2:8 isemayo kuwa:-
"Mkumbuke, Yesu Kristo, aliye fufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo Injili yangu. 2Wafalme 2:8."
Ilikuwa ni kazi kweli kweli upande wake Ismail, koo lilikuwa limemkauka, alikunywa maji kiasi kutuliza ukavu wa koo lake, kisha alisema kuwa:
Mambo ya ufufuo katika Marko 19:9-20 yameondolewa katika Biblia nyingi. Kama bado zimo, itakuwa zimewekwa kwa maandishi madogo madogo ama zipo kwenye mabano na maelezo yake yameoneshwa chini ya ukurasa. Aliwaambia waangalie katika Revised Standard Version, New American Standard Bible na New World Translation of the Holy Scripture.
Ustadhi aliwauliza iwapo Yesu aliwahi kudai, yeye ni Mungu au kusema mimi Mungu wenu niabuduni?
Kahin kama kawaida yake, alidakia tena na kukiri kuwa Yesu hakusema hivyo, ila alisisitiza kuwa Yesu ni Mungu pia ni binadamu.
Ustadhi alimuuliza Kahin iwapo Yesu aliwahi kudai hivyo? Kahin alijibu kuwa hakuwahi. Hapo ndipo Ustadhi alimthibitishia katika Mathayo 15:9 kwamba:-
"Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Mathayo 15:9."
"Ustadhi alizidi kuwaambia wapwa zake huku akiweka msisitizo wa aya kadhaa za Biblia, alisema hivi:-
"Itikadi na imani zote za Ukristo wa leo ni zao la fikra za mwanadamu, kama vile utatu, Yesu mtoto wa Mungu, Yesu ni Mungu, Dhambi ya asili na kafara. Yesu kwa kauli yake hakudai hayo.
Yohana 8:28 inasema: Baba Mkuu kuliko mimi. Yohana 14:28 inasema: Bwana Mungu wetu ni Bwana mmja. Marko 12:29 inasema: Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Marko 15:34 inasema: Ee baba, mikononi mwako naiweka roho yangu. Luka 23:46 inasema: Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye hata Malaika walioko mbiguni, wala mwana ila Baba."
"Hivyo basi, kwanza Yesu aliitwa Mtume, kisha Mwalimu kutoka Mungu, halafu mtumishi wa Mungu, tena Masihi, akapandishwa na kuitwa mtoto wa Mungu, na baadae akaitwa Mungu. Tumieni akili zenu, vipi Mungu azaliwe na kiumbe mwingine yeyote yule?"
"Yesu alikuwa akilala, Mungu halali tazameni Zaburi 121:4."
"Yesu alimwabudu Mungu, tazameni Luka 5:16."
"Mungu ni mwenye nguvu na uwezo."
"Sasa nawaulizeni: Vipi watu wamtemee mate na kumsulubu? Vipi awe Mungu iwapo yeye alimwabudu Mungu? Vipi ajaribiwe iwapo Mungu hajaribiwi? Tazameni Yakobo 1:13.
Wakati Ustadhi anafafanua maandiko hayo, hakuna aliye thubutu kuuliza swali wala kutoa hoja.
Bali papo kwa papo yaani Kahin alithubutu kusema kuwa, ni kweli yeye binafsi anashindwa kufahanu, basi labda wakubali hivyo hivyo.
Lakini Ustadhi alimfahamisha Kahin kuwa, itakuwa anakwenda kinyume na Biblia inayotutaka tupime kila jambo. Aliwataka wasome 1Wakorintho 5:21 itawaambia.
Pamoja na maelekezo hayo lakini Kahin alijibu kwa ufupi tena akiwa kama vile kachukia kuwa, aliona ni machafuko kwake.
Ustadhi baada ya kumuona Kahin kuwa kachukia kama vile imekuwa ni kashifa kwake, hakumwacha hivi hivi. Alimalizia kwa kumwambia kuwa, machafuko atayaleta yeye menyewe, kwa imani yake ya kibinadamu. Aliwataka wengine waisome 1Wakorintho 14:33 inayosema:-
"Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, vile vile kama alivyo katika makanisa yote ya watakatifu."
Njaa ilitawaliwa na mazungumzo, hakuna aliyedai anajisikia njaa. Walishitukia jua limeisha kuchwa na kiza kinakaribia kuenea. Waliahirisha mazungumzo hadi Siku iliyo fuata.
Sura ya "10"
Siku hiyo iliyofuata, mjadala ulianzishwa na Adul kwa kuuliza awali:-
"Je, Yesu ni mtoto wa Mungu?"
Bila kukawia Kibon aliingilia kujibu kwamba ni ndiyo kwa mujibu wa Mathayo 3:17 isemayo:-
"Na tazama sauti kutoka Mbinguni ikisema, huyu ni mwangu, mpendwa wangu, nimependezwa naye."
Adul aliwaelesha kuwa, ni sawa, ila wasikubali tu neno kwa maana ya kawaida, Mitume pia na watu wa kawaida, tumeitwa wana wa Mungu katika Biblia Kutoka 4:22.
Pamoja na hayo, aliendelea kutoa hoja kuwa, mbona kuna aya isemayo:-
"Nawe Musa umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israel asema hivi, Israeli ni mwangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu."
Adul alimwambia Kibon kuwa asubri kwanza amueleweshe, ilikuwa hivi:-
"Mtoto wake wa kwanza ni Yakobo ambaye ni Israeli. Tazama 1Mambo ya Nyakati 22:10.
Kibon alikanusha na kusema kuwa huyo ni Selemani atakaye jenga nyumba kwa ajili ya jina langu, naye atakuwa mwanangu nami nitakuwa babaye. Adul alizidi kumpa somo kuwa asome Yeremia 31:9 isemayo:-
"Mimi ni baba wa Israeli, na Efrahimu ni mzaliwa wa kwanza wangu."
Adul aliwauliza kuwa, ni nani mzaliwa wa kwanza Israeli au Efrahimu? Kwani watu wa kawaida nao ni watoto wa Mungu. Aliwaambia wasome Kumbukumbu la Taurati 14:1 isemayo:-
"Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu."
Adul alizidi kuwaelewesha kuwa, watu wa kawaida nao wameitwa watoto wa Mungu. Aliwaambia wasome Warumi 8:29 isemayo kuwa:-
"Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi."
Adul aliwauliza, iwapo ni watoto wa kwanza, Yesu atakuwa vipi tena ?"
Kibon aliingilia na hapo akasema kuwa:-
"Yesu ni mwana pekee aliyezaliwa na Mungu."
Adul kwa makini sana, alianza kumfahamisha Kibon kwamba:-
Kwanza, kabla ya Yesu hajazaliwa miaka mingi iliyopita, Mungu alimwambia Daudi katika Zaburi 2:7. Alimuomba Kibon awasomee:-
"Zburi 2:7 inasema hivi, Nitaisubiri amri, Bwana aliniambia Daudi, ndiwe mwanagu, mimi leo nimekuzaa."
Adul aliendelea kuwajuza. Aliwaambia wapwa zake, waangalie, Daudi naye mtoto aliyezaliwa na Mungu. Hivyo neno mtoto w Mungu katika Biblia halitumiki katika maana yake halisi, ila hutumika kifumbo au kimethali. Kwa hiyo basi mtoto wa Mungu anawea kuwa yeyote yule anaye pendwa na Mungu. Yesu vile vile amesema kuwa Mungu si Baba yake tu bali ni baba yenu. Alimwambia tena Kibon awasomee Mathayo 5:45-48.
"Mathayo 5:45-48 inasema hivi, Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu, na basi ninyi mtakuwa wakamilifu kama baba yenu wa Mbiguni alivyo mkamilifu."
Hivyo basi, Adul alizidi kusema, utaona aya nyingi ndani ya Biblia neno 'mwana' wa Mungu hutumika kwa maana ya upendo, huba, ukaribu na Mungu, na halimhusu Yesu peke yake, pia utaona Mungu ana watoto wa kike na kiume.
Adul kwa mara nyingine alimwamuru Kibon awasomee 2Wakorintho 6:18.
"2Wakorintho 6:18 inasema hivi, Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu, asema Bwana Mwenyezi.".
Adul aliendelea kuwaambia kuwa, aya hiyo na nyingine nyingi ndani ya Biblia hazina maana ya kuwa Yesu ni mtoto pekee.
Kibon alichukua kikombe chake cha maziwa akanywa mafundo kama mawili hivi ndipo aliposema kuwa, Yesu hana Baba, hivyo ni mtoto wa Mungu.
Adul alimuuliza Kibon kuhusu Adamu ilikuwa vipi? Alimwambia awasomee Lukan 3:38 na Waebrania 7:3:-
"Luka 3:38 inasema hivi, Wa Enoshi wa Sethi, wa Adamu wa Mungu."
"Waebrania 7:3 inasema hivi, Hana Baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo na siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na mwana wa Mungu, huyo adumu kuhani milele."
Adul aliwapasha kuwa huyo anaye zungumziwa je, wanamfahamu? Kibon alijibu kuwa hapana. Ndipo alipomwabia awasomee Waebrania 7:1:-
"Waebrania 7:1 inaasema hivi Melkizedeki huyo mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu........."
Adul aliwauliza kuwa, je hawaoni aliye pekee zaidi kuliko hata Yesu na Adamu. Mbona yeye hawamchukulii ni mtoto wa Mungu au Mungu?
Wote walibaki kimya huku wakitafakari nini cha kujibu. Lakini hapakuwa na jibu lolote. Bali Kibon alitaka kujua kuwa, Waislamu Yesu wanamwita nani?
Alijibiwa kuwa Yesu, Waislamu humwita Yesu mwana wa Mariamu. Adul aliwauliza iwapo kuna ambaye anapinga hilo?
Hapakuwa na ubishi, Adul aliendelea kuwajuza kuwa, Yesu mwenyewe amejiita mwana wa Adamu na akakataa kuitwa kuitwa mwana wa Mungu. Alimtaka Kibon awasomee Luka 4:41, Luka 9:20 na 21_ Yohana 6:14 na Yohana 3:2:-
"Luka 4:41 inasema hivi, Pepo nao waliwatokea watu wengi, wakipiga kelele na kusema, wewe umwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiyo Kristo."
"Luka 9:20-21 inasema hivi, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo mwana wa Mungu. Nawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo."
"Yohana 6:14 inasema hivi, Basi wale watu walipoiona ile ishara aliyoifanya, walisema, hakika huyu ni Nabii yule ajae ulimwenguni."
"Yohana 3:2 inasema hivi, Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi twajua kuwa umwalimu umetoka kwa Mungu."
"Matendo ya Mitume inasema hivi, Mara akahubiri Yesu katia Masinagogi, kwamba yeye ni mwana wa Mungu."
Adul aliwashereheshea maandiko hayo yalikuwa na maana kuwa Yesu alikataa kuitwa mwana wa Mungu. Hata wanafunzi wake aliwaonya wasimwite hivyo.
Pili, aya hizo zinasadikisha kuwa Yesu siyo mwana pekee wa Mungu, yeye ni masihi anayesubiriwa, tena ni Nabii, akaitwa Mwalimu, baadae mwana wa Mungu, Bwana kisha Mungu.
Adul aliendelea kuwaelewesha kuwa, aya hizo zipo wazi, hana la kuongeza, ila jambo jingine ni kuwa, Wakristo wa mwanzo walikuwa wakitumia Masinagogi. Baadae Ukristo na mafundisho ya Yesu yalipotoshwa na kutupwa. Paulo na Barnaba walio na vyeo walifukuzwa katika Masinagogi na kushutumiwa kuwa ni makafiri na wachafuzi. Ushaidi upo katika Matendo 13:50, 17:18, Luka 2:11 na Yohana1:1. Alimtataka Edward awasimee aya hizo.
Kibon alijitengeneza vizuri akaagalia kikombe chake cha maziwa, lakini maziwa yalikuwa yameisha bila kufahamu. Kisha alianza kuzisoma aya hizo:-
"Matendo 13:50 inasema hivi, Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watumwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao."
"Matendo 17:18 inasema hivi, Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wenhine wakasema , mpuuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, anaonekana kuwa mtangaza habari za Miungu migeni kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo."
"Nyinginene inasema hivi, Wakapiga kelele na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiyo mtu wa yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na pahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaagiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi pahali hapa patakatifu."
"Luka 2:11 inasema hivi , Maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, mwokozi ndiye Kristo Bwana."
"Yohana 1:1 inasema hivi, Hapo mwanzo kulikuwa na neno, Naye neno alikuwako kwa Mungu, Naye neno alikuwa Mungu."
Mazungumzo yalisitishwa kwa muda mchache ili kutoa nafasi kwa wazungumzaji kujijenga upya na pia kumaliza shida ama haja zao. Baada ya hapo waliendelea na mazungumzo yao.
Sura ya "11"
Siku iliyofuata walikaa kuendelea na mazungumzo yao. Safari hii alianza mjomba wao Ustadhi kwa kuwapa swali iwapo wanaamini kuwa Yesu aliuawa msalabani?
Moja kwa moja mpwaye Kitin alikubali kuwa, ndiyo alikufa kisha akafufuka.
Ustadhi alimwambia kuwa wao Waislamu wanaamini hakufa msalabani kwa ushahidi wa Qur'an sura ya 4:157 isemayo kuwa:-
"Na kwa kusema kwao Mayahudi-sisi tumemuua masihi Isa, mwana wa Mariam Mtume wa Mungu, hali hawakumuua wala hawakumsulubu."
Kitin aliuliza zaidi kutaka kujua:-
"Lakini je katika swala la kufufuka?"
Ustadhi naye ilibidi kabla ya kujibu hoja aliyopewa alimuuliza swali:-
Wote kwa pamoja walikubaliana na hilo. Ndipo aliendelea kuwaelemisha kwamba, waliona kaburi ambamo Yesu alilazwa likiwa tupu, wao wakachukulia amefufuka, kwa sababu tu wanafunzi na mashahidi wengine walimuona tena yu hai baada ya lile dai la kusulubiwa.
Kitin alijitutumua kuonesha kuwa Biblia anaielewa vizuri alimpa swali:-
"Je, unao ushahidi wowote ule?"
Ustadhi alitoa jibu kwamba iwapo Biblia ikituthibitishia, je, hàbari ya nani utazipa uzito? Ya Yesu wanafunzi walivyoyasikia au ya wafuasi na mashahidi wengine?
Moja kwa moja Kitin alitoa jibu kuwa atazipa uzito habari za Yesu.
Ustadhi alikubaliana naye kwa kusema kuwa, Mwanafunzi hampiti Mwalimu wake n wala mtumwa hampi Bwana wake. Mathayo 10:24.
Kitin alizidi kuweka msisitizo kutoa hoja kwamba Yesu alisema kuwa atafufuka katika Luka 24:46.
"Luka 24:46 inasema hivi, Akamwambia, ndivyo ilivyoandikwa kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu."
Ustadh hakuchoka. Alizidi kuchambua na kufafanua kuwa, neno kuteswa limetiwa chumvi ndani ya biblia na kuitwa kufa. Katika 1Wakorintho 15:31 Paulo alsema:-
"1Wakorintho 15:31 inasema hivi, Paulo alisema: Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu kuliko nako juu ya Yesu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa." Yaani ninateseka kila siku.
Adul alipepesa macho yake huku na kule, kuwaangalia iwapo wanafuatilia na kuzingatia. Kisha aliwataka wamvumilie kwa maelezo marefu ambayo anataka kuyatoa muda siyo mrefu. Alianza kusoma:-
"Ufuatao ni baadhi ya ushahidi. Kwanza Yesu alipokuwa msalabani, alimuomba Mungu ifuatavyo:- Mungu wangu Mungu wangu mbona unaniacha?" Mathayo 27:46.
"Kisha akasema Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako,uniondolee kikombe hiki, walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke." Ina mana kikombe cha mauti.
"Pili, Dua zake au kuomba, kwake kulikubaliwa. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Ina maana Malaika alimhakikishia kwamba Mungu hatamwacha bila ya kumsaidia. Luka 22:43."
"Nayo Waebrania 5:7 Yeye siku hizo za mwili wake, alimtokea yule, awezaye kumuomkoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu. Ina maana maombi yake yalipokelewa."
"Yakobo 5:16.......kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."
"Mathayo 7:7-10 Ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa, kwa maana kila aombaye hupokea, naye atafutaye huona naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye mwanaye akimuomba mkate atampa jiwe? Au akiomba samaki atampa nyoka? Hapa ni Yesu mwenyewe anafundisha. Sasa vipi inashikiliwa tu kwamba amekufa msalabani?"
"Tatu,Askari hawakuvunja miguu yake. Basi askari wakaenda, wakavunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulubiwa pamoja naye. Lakini walipomwijia Yesu na kuona kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu. Yesu hakuwa na hatia. Ilikuwa ni mbinu ya askari kumuokoa Yesu. Yohana 19:32,33."
"Nne, Yohana 19:34 Lakini askari mmoja wapo alimchoma ubavuni kwa mkuki, na mara ikatoka damu na maji." Huu ni uongo, Yesu angekufa msalabani damu yake ingeganda.
"Tano, Mathayo 12:40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la Nyangumi, hivyo ndivyo mwana wa Adamu atakavyo kuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa wa nchi." Hapa ni waandishi na mafarisayo walipomtaka Yesu ishara. Mbali na hayo siku tatu hazikutimia, ilikuwa mchana mmoja wa jumamosi tu na usiku wa jumamosi na jumapili basi. Lakini je Yona alikuwa mzima katika tumbo la Nyangumi?"
Kitin alikurupuka haraka haraka kutoa jibu kwamba Yona alikuwa mzima. Naye Adull akapata nafasi ya kumuuliza kuwa je Yesu nae alikuwa hai kama alivyosema? Alishindwa kujibu. Kisha aliendelea:-
Sita, Yohana 20:17 Usinishike kwa maana sijapata kwenda kwa baba......." Ina maana pengine angemtonesa vidonda vyake, pia sijapata kwenda kwa Baba, ilikuwa bado hajafa yupo hai. Mtu anapo kufa anarejea kwa muumba wake.. Hivyo ni ushahidi kamilifu alioutoa Yesu mwenyewe.
"Saba, Wanafunzi wake walidhania kuwa Yesu yule yule wa mwili, bali alikuwa wa Roho'mzimu' kwa sababu mwili ulio kufa huwa ni roho.
Kitin alihoji uhakika wa maandiko hayo. Ustadhi alimjibu kuwa Yesu ndiye aliyesema katika Biblia kuwa, kuna miili huwa sawa na Malaika. Kitin alitaka uthibitisho ndani ya Biblia apewe. Akaambiwa awasomee Luka 20:34-36.
"Luka 20:34-36 inaesema hivi, Yesu akamwambia, wana wa ulimwengu huu huwa na kuelewa lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawa sawa na Malaika, nao ni wana wa wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo."
"Luka 24:36-41 inasema hivi, Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu. Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhaniya kwamba wanaona roho. Akawaambia, mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikeni shikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayo aliwaonesha mikono na miguu Yake. Basi walipokuwa hawajaamini, kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, mna chakula chochote hapa? Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa, akala mbele yao." Hii iliku ni kuwathibitishia kuwa anakula kama binadamu mwingine.
Nane, Kumbukumbu la Taurati inasema hivi, Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa naye ukamtundika juu ya mti; mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti, lazima utamzika siku hiyo hiyo, usije ukatia unajisi katika nchi yakoa akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako."
Kwa mjibu wa aya hiyo kama bado mnaamini Yesu alikufa msalabani, basi alikuwa ni Nabii wa uongo na amelaniwa na Mungu. Pia ni kutosadiki utume wake, Mayahudi walishikilia kwamba wamemuua Yesu msalabani ili kuonyesha kuwa alikuwa ni muongo dhidi ya madai ya utume. Wakristo wanaamini, ili uokoke na dhambi ni sharti uamini, Yesu alikufa msalabani. Hii ni kukubali kuwa Yesu alilaniwa. Hata imani hiyo inapingana na mafundisho ya Biblia katika Hosea 6:6 isemayo:-
Maana nataka fadhila wala si sadaka, na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
Pia, Mathayo 9:13 isemayo hivi, Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka."
Kitin aliingilia kati na kusema kuwa ama kuuliza, inakuaje baadhi yao wanaamini kufufuka kwa Yesu? Hapo hapo Adul alimjibu kuwa ni Paulo ndiye aliyefundisha Imani hii kama alivyoielezea huko nyuma katika baadhi aya ya Matendo 17:18, 2Timotheo 2:8 na Matendi 9:20.
Lakini bado Kitin alikuwa anahoji kuhusu Marko 16:19 kwamba, Yesu alichukuliwa mbiguni na akakaa mkono wa kulia wa Mungu.
Ustadhi alimwambia Kitin kuwa, aya katika Marko 16:9-20 zimeondolewa katika baadhi ya Biblia. Hayo aliisha mwambia walipo kuwa kwenye mjadala wa Biblia Takatifu. Kama bado anaamini hivyo mbona hakubali kuwa Mitume wengine kuwa ni Miungu kwa sababu walichukuliwa nao mbiguni?
Kitin aliuuliza ni Mitume gani hao. Jibu alipewa kuwa awasomee 2Wafalme 2:11-12, Mwanzo 5:24 na Waebrania 11:5:-
"2Wafalme 2:11-12 inasema hivi,...... Naye Eliya akapanda Mbiguni kwa upepo kwa upepo wa kisulisuli......wasimwone tena kabisa."
"Mwanzo 5:24 inasema hivi, Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa."
"Waebrania 11:5 inasema, Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha, maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu."
Ilikuwa ni muda wa kupata chakula cha mchana, kila mmoja alikuwa amechoka kiakili, hivyo basi ilibidi wapumzike kwanza.
Sura ya "12"
Kilifuata kipindi kingine baada ya chakula cha mchana. Walianza mazungumzo yao. Kahin aliibuka na hoja ya kwamba, ina maana, kuokoka na dhambi kwa kuamini ufufuo. Je, siyo mafundisho ya Yesu?
Ustadhi alimwambia Kahin awasomee Kumbukumbu 24:16, Yeremia 31:30 na Ezekiel 18:20:-
"Kumbukumbu 24:16 inasema hivi, Mababa wasiuwawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuwawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auwawe kwa ajili ya dhambi yake mwenewe."
Yermia 31:30 inasema hivi, Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe."
" Ezekiel 18:20 inasema hivi, Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwane, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenyewe utakuwa juu yake."
Ustadhi aliwafahamisha kuwa, hivyo basi, Adamu na Hawa wana jukumu lao wenyewe kwa makosa yao ambayo walisamehewa baadae kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.
Imani ya kafara, ilikubaliwa na Kanisa baada ya kuondoka Yesu Duniani, miaka mitatu na mia nne iliyopita.
Kahin alisema kuwa aya hizo zimo kwenye Agano la Kale. Ustadhi alimkubalia kuwa ni sawa, ila sasa awasomee Mathayo 7:1 na 2 kisha 1Wakorintho 3:8:-
"Mathayo 7:1 na 2 inasema hivi, Msihukumu mkaja mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo ndiyo mtakayo hukumiwa; na kipomo kile kipimacho, ndicho mtakacho pimiwa."
"1Wakorintho 3:8 inasema hivi, Basi yeye apendaye, na yeye atiaye maji ni mmoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawa sawa na taabu yake mwenyewe."
Tena Kahin alitaka athibitishiwe je, watoto huzaliwa bila dhambi? Ustadhi alimwambia Kahin awasomee Mathayo 19:14:-
"Mathayo 19:14 inasema hivi, Lakini Yesu akasema waacheni watoto wadogo waje kwangu, wasiwazuie, kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbiguni ni wao."
Usitadhi alizidi kumwelewesha na kuwauliza kuwa, wameona, kwamba watoto huzaliwa bila dhambi. Tena wanajua kwamba Torati ambayo ni sheria ya Musa ilivunjwa na Paulo?
Lakini Kahin alitaka kujua ni aya gani hiyo. Ustadhi alimwambia awasomee Matendo 13:39:-
"Matendo 13:39 inasema hivi, Na kwa yeye kila amwaminie huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa."
Hapo ndipo Ustadhi alipowauliza, iwapo Paulo, hakumuona Yesu akiwa hai, na anakiri hii ilikuwa injili yake, kwa nini wao wanaamini Yesu alifufuka?
Kahin alihoji hayo yameandikwa wapi? Ustadhi alimwambia awasomee 2Timotheo 2:8.
"2Timotheo 2:8 inasema hivi, Mkumbuke Yesu Krito, aliye fufuka kutoka wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu."
Ustadhi aliwageukia kisha aliwauliza iwapo bado wana haja ya kuamini kuhusu kusulubiwa na kufufuka katika wafu?
Alizidi kuwapa somo kwamba, Uislamu ni dini ambayo kiakili inakubalika na mafundisho yake yasiyo changanyika na ukafiri wala imani nyingine za kishirikina.
Mara Kahin alitoa kauli kuwa, hayo ndiyo wao wanayo yatafuta. Ustadhi aliwauliza kwa nini hawataki kutamka SHAHADAH?
Kibon naye alikiri kuwa wao hawajui kutamka. Ustadhi aliwaambia kuwa atawasaidia kutamka na kisha wamfuatishe yeye. Ustadhi alianza kutamka na kuendelea:-
"Ninakiri kuwa, hapana Mungu anayestahiki kuabudiwa, ila Allah na nakiri kuwa, Muammad ni mtumishi na Mtume wake. Ash hadu an la Illah illal lahu wah dahuu la sharika lahu, wa ash hadu anna Muhammadan abuduhu wa rasuluhu."
Baada ya kukiri huko palikuwa na minong'ono ya hapa na pale, ndipo Kahin aliuliza iwapo Mtume Muhammad alitabiriwa ndani ya Biblia.
Ustadhi alimpa jibu kuwa, Mtume Muhammad alitabiliwa, ila kwa Muislamu siyo lazima kuyafahamu toka kwenye Biblia. Lakini kwa kuwa una ujuzi na Biblia, tuta zungumza nanyi wakati mwingine tukijaliwa ingawa kwa ufupi tu.
Kabla hawajaendelea na mjadala wao, siku ambayo walikiri na; kutamka ashahadah. Kwa maana ya kusilimu na wakawa Waislamu. Ustadhi aliwataka watamke majina waliyo chagua.
Wa kwanza alikuwa Kibon alichagua jina aitwe Abubakar.
Pili alikuwa Kahin alitlaka aitwe jina la Hussein.
Wa tatu alikuwa Katin alitaka aitwe Suleiman.
Wa mwisho alikuwa Love yeye alichagua jina la Zainab.
Sura ya "13"
Siku iliyofuata mazungumzo yaliendelea kama kawaida.. Mjadala ulikuwa juu ya Muhammad kutabiriwa ndani ya Biblia. Naye Abubakari (Kibon) alianza kwa kusema:-
"Mjomba, mbona mama yetu hatujamsikia kuongea, atujui yuko upande gani?"
Zainab (Love) alishituka sana, alipo sikia ujumbe ulio muhusu yeye ukitajwa na mwanae. Kuna usemi, maji ukiyavulia nguo inabidi uyaoge. Alijieleza yeye mwenyewe:-
"Kaka, wanangu, huu ndio ukweli wangu. Udanganyifu wa maisha, ndiyo ulio nifanya Niitwe jina hilo. Mimi jina langu halisi ni Amina, mimi ni Muislam."
Abubakar (Kibon) alimjibu mama yake kuwa wamemwelewa hivyo basi waendelee na mjadala wao. Ndipo Ustadhi aliwauliza wapwaye:-
"Je mnafahamu kwa nini Ishmail na mama yake Hajir waliondoka kwa Sarah?
Abubakar (Kibon) alijibu bila hata kuwa na wasiwasi kuwa:-
"Waliondoka kwa sababu, Sarah hakutaka Ishmail awe mrithi pamoja na Isaka. Pia Ishmail alifanya dhihaka."
Ustadhi alimsifia mpwaye kwa jibu alilojibu, kwamba ni vizuri sana na kisha alinukuu aya hiyo kuwa ni Mwanzo 21:8-10, aliisoma:-
"Mwanzo 21:8-10 inasomeka hivi, Mtoto akakua akaachishwa kunyonya. Ibrahim akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipo achishwa kunyonya. Sarah akamuona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahim, anafanya dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu mfukuze mjakazi huyo na mwanae, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka."
Hivyo ndivyo inavyo nena ni sahihi kabisa Suleiman (Kitin) alisisitiza. Naye Ustadhi alitwaa kitambaa cha mkono kutoka mfukoni mwake, akajifuta jasho usoni mwake kisha akasema:-
"Sikilizeni kwa makini, Mwanzo 16:16 inatuambia kuwa. Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita. Hapo alipomzalia Abrahamu Ishmaili."
"Sasa tuone Mwanzo 21:15 nayo inatufahamisha ya kuwa, Naye Ibrahimu likuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka."
Ustadhi aliwauliza kuwa hawaoni Mwanzo 21:8-10 inapingana na Mwanzo 21:14-21 ?" Lakini hawakuweza kuliona kwa wakati huo. Ilibidi awasomee:-
"Inasema hivi, Ibrahimu akaamuka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana akamruhusu, naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer Sheba. yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijti kimoja. Akaenda akakaa akimkabiri, mbali naye kadri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbiguni, akamwambia, una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akajaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jagwa, akawa mpiga upinde. Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Suleiman (Kitin) aliuliza aya hiyo inawaeleza nini na utofauti wake ni nini? Ustadhi aliwajibu hivi:-
"Kwanza ieleweke, Isaka alipo achishwa kunyonya alikuwa na miaka miwili ya kuzaliwa kwake. Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka kumi na sita. Pia Ibrahimu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita alipozaliwa Ishmaeli. Hali kadhalika Ibrahimu alitimiza miaka mia moja ndipo Isaka akazliwa."
"Pili, hivyo basi inaonekana wazi kuwa, Hajiri na mwanae Ishmaeli walikwisha ondoka siku nyingi kabla hata Isaka hajazaliwa."
"Katika mafundisho ya Kiislam tunasema: Ibrahimu alimchukua Ishmaeli na Hajiri akawapa makazi mapya katika mji wa Makka ambapo katika Biblia umeitwa Parani, na alifanya hivi kwa kumtii Mwenyezi Mungu."
"Katika vilima vya Safa na Marwa ni kati vilima alivyo kwenda Hajiri mara kadhaa akitafuta maji. Baadae ikawa ibada moja wapo ya Kiislamu inayofanywa kila mwaka yaani Hija.
"Kisima kilicho tajwa ndani ya Biblia, hadi leo kipo kinaitwa Zamzam."
"Ibrahim na Ishmaeli walijenga Kaaba katika mji wa Makka, mahali ambapo Nabii Ibrahimu (a.s.) alikuwa akifanyia ibada karibu na kaaba nayo ipo hadi leo inaitwa MAGAMMU IBRAHIMU. Ndiyo asili ya kuadhimisha kwa mahujaji na wengine, kwa kujitoa muhanga, Nabii Ibrahimna mwanae Ishmaeli, kwa kuchinja wanyama."
Baada ya maelezo marefu yaliyo tolewa na Ustadhi na kuonekana yameeleweka . Suleiman (Kitin) hakusita kusema:-
"Lakini inasemekana kwamba na kuaminika kuwa Isaka ndiye alitakiwa kutolewa muhanga."
Ustadhi alikana kisha alitoa maelezo kuwa siyo kweli, aliwarejesha katika Mwanzo 17:24-27 inayotuambia:-
"Mwanzo 17:24-27 inasema kuwa Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipo tahiriwa nyama ya govi lake. Ishmaeli mwanae alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu alipotahiriwa nyama ya govi lake. Siku ile ile akatahiriwa Ibrahim na Ishmaeli mwanae. Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na waunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye."
Husein (Kahin) aliomba wapatiwe ufafanuzi, kwani bado haijaeleweka. Ustadhil aliwafafanulia:-
"Ni kwamba, Uislamu unasema, Agano maana yake ni ahadi. Agano lilikuwa kati ya Mungu, Ibrahimu na Ishmaeli aliyekuwa mwanae pekee kwa wakati huo. Kipindi hicho Isaka alikuwa hajazaliwa. Ndiyo siku alitaka kutolewa muhanga walitahiriwa wote."
Zainab (Love) naye alitoa hoja kwamba bado hajaelewa, hivyo anaomba ufafanuzi zaidi. Ustadhi aliendelea na ufafanuzi:-
"Ni hivi, lilipo wekwa Agano na kuthibitishwa kwa kutahiriwa pamoja na kujitoa muhanaga. Ibrahimu alikuwa na miaka tisini na tisa, Ismail alikuwa na miaka kumi na mitatu. Mwaka mmoja baadaye akazaliwa Isaka wakati Ibrahimu anatimiza miaka mia moja."
"Hivyo basi Ishmaeli na uzao wake, Mtume Muhammad (s.a.w.) na Waislam wote, wanatekeleza Agano la kutahiri, pia sala vipindi vitano kwa siku na kumtakia rehema Nabii Ibrahimu na kizazi chake."
Abubakari (Kibon) alikuwa bado na hoja, katika Mwanzo 22: Kwamba Isaka alikuwa atolewe muhanga. Ustadhi aliendelea na ufafanuzi:-
"Nafahamu, imetajwa hivi, Mwana wako wa pekee, umpendaye, ISAKA. Kwa nini isiandikwe 'mwana wako wa pekee umpendae Ishmaeli?' Ishmaeli alikuwa na miaka kumi na tatu, Isaka alikuwa bado hajazaliwa. Ndiyo kusema jina la Ishmaeli limeondolewa na kuwekwa la Isaka katika mwanzo 22: yote. Lakini Mwenyezi Mungu amelihifadhi neno PEKEE kutuonesha lilikuwa limekusudiwa nini hasa. Ukisoma maneno 'nitauzidisha uzao wao' katika Mwanzo 22:17, yalitumiwa kwa Ishmaeli katika Mwanzo 16:10. Sasa hamuoni Mwanzo 22: yote inamhusu Ishmaeli? Pia nenno ' Nitamfanya kuwa Taifa kubwa mara mbili yanamtaja Ishmaeli katika Mwanzo17:20 na Mwanzo 20:18 hayakutumika kabisa kwa Isaka."
Abubakar Kibon) alisema kuwa bado Wakristo na Mayahudi wanaamini kuwa Isaka ni bora kuliko Ishmael.". Pamoja na hayo Ustadhi alimwambia Abubakari (Kibon) amsikilize:-
"Sikiliza, wao ndiyo wasemavyo, ila Biblia Mwanzo 15:4 inatueleza hivi, Nalo Neno la Bwana likamjia akanena, huyu yaani Eliezeri Mdameski hatakurithi; bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakaye kurithi." Hivyo Ishmael alikuwa ni ni mrthi pia.
"Abubakar (Kibon) alitaka kujua kuhusu kubarikiwa inakuwaje? Ustadhi hakuchoka aliendelea kuafafanulia:-
"Zipo aya ndani ya Biblia zinathibisha ubarikiwa wa Ishmael, ya kwanza ni Mwanzo 16:10 inatueleza, Malaika wa Bwana akamwambia, hakika nitakuzidishia uzao wako, wala hautahesabiwa kwa jinsi utakavyo kuwa mwingi.
" Mwanzo 17:20 inasema, Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidishia nami nitamuongeza sana sana. Atazaa maseydi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa Kuu."
Ustadhi aliwauliza iwapo kama bado hawajaridhika na maadiko hayo. Naye Hussein (Kahin) alijibu kuwa bado hawajaridhika. Ustadhi akaamuru wasome Mwanzo 21:13, na 21:18 pia Kumbukumbu 21:15-17:-
"Mwanzo 21:13 inanasema , Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa Taifa, maana huyu naye ni uzao wako."
"Mwanzi 21:15-17 inasema, Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa."
"Kumbukumbu 21:15-17 inasema, Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzliwa wa kwanza akiwa ni wa mke. asiyependwa. Ndipo itakapo kuwa kwamba siku atakayo waridthisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana asiyependwa, naye ndiye mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake, haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye."
Ustadhi aliwauliza kwa mara nyingine iwapo wameelewa au bado. Wote kwa pamoja waliitikia kuwa wameielewa. aliendelea kuwaelewesha:-
"Hivyo basi, Uislamu haukatai kuwa Isaka na kizazi chake wamebarikiwa, la asha, isipokuwa tunasema, mtoto wa Agano ni Ishmaeli, na Mtume wa mwisho wa Mitume yote Muhammad (s.a.w.) ndiye aliyetokana na naye."
Zainab (Love) naye alitoa lake kuwa, wanavyo dai Wakristo na Mayahudi, Ishmaeli ni mtoto wa Haramu. Ustadhi aliendelea kuwafahamisha:-
"Sawa, lakini Biblia haisemi hivyo, itakuwaje Mtume mkubwa kama Ibrahim atakuwa na mke asiye halali na kupata mtoto nje ya ndoa?"
Wote walikaa kimya hakuna aliyejaribu kujibu swali hilo. Ndipo Ustadhi akasema wasome Mwanzo 16:3 na 20:12 pia 16:11:-
"Mwanzo 16:3 inasema, Sarai mkewe Abraham akamtwaa Hajiri. Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abrahamu katika nchi ya Kaanani miaka kumi, akampa Abrahamu mumewe awe mkewe."
"Mwanzo 20:12 inasema, Naye kweli ni ndugu yangu, binti ya baba yangu ila asiye mwana wa mama yangu ndipo akawa mke wangu."
"Mwanzo 16:11 inasema, Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama, wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako."
Ustadhi aliwauliza iwapo Biblia imeweka bayana kuwa wapi Ishmael ni mtoto wa haramu? Abubakar (Kibon) alijibu kuwa hakuna palipo andikwa, aliendelea:-
"Hivyo basi Ishmaeli maana yake ni Mungu anasikia. Pia Mwenyezi Mungu aliweka Agano na Abramu kabla hata Ishmael na Isaka kuzaliwa."
Zainab (Love) aliuliza ni aya ipi hiyo? Ustadhi aliendelea kuwafahamisha:-
"Mwanzo 15:18 inatuambia Siku ile Bwa na akafanya Agano na Abramu, akasema, uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka mto huo mkubwa, mto Farati."
Baada ya hapo, Ustadhi aliwauliza iwapo sehemu kubwa ya Arabuni ipo baina ya mto Nile na Flati ambako ndiko walikaa uzao wa Ishmaeli?
Hapakuwa na hata mmoja aliyejibu, walionekana kuchoka, pia njaa ilikuwa imeisha washika.
Hussein (Kahin) alitaka kujua iwapo Isaka na uzao wake, hawakuahidiwa nchi yoyote?
Ustadhi aliwafahamisha kuwa Waislamu hawasemi hivyo, aliwaomba wasome Mwanzo 17:8
"Mwanzo 17:8 inasema, Nami nakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kaanani, kuwa miliki ya milele, nami nitakuwa Mungu wao."
Ustadhi aliendelea kuwajuza kuwa Ibrahim anakaa ugenini katika nchi ya Kaanani na wala siyo nchi baina ya mto Nile na Farati; kwa kuwa Chldean alikuwa Mwarabu zaidi kuliko Myahudi.
Hapo hapo Hussein (Kahin) alisema kuwa, kwa mujibu wa Mwanzo 17:21 Agano liliwekwa kwa ajili ya Isaka. Ismail aliomba wasome aya hiyo:-
"Mwanzo 17:21 inasema, Bali Agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sarah atakuzalia majira kama haya mwaka ujao."
Ustadhi alihoji kuwa ni vipi aya hii inamtoa Ishmael. Bibilia imesema wapi kuwa, hataweka Agano na Ishmail?. Hussein (Nebort) alijibu kuwa hakuna.
Walikuwa kimya wanamsubiri mjomba wao atoe ruhusa ya kuahirisha mazungumzo yao. Lakini alotokea Abubakar (Kibon) akasema:-
"Mjomba, sisi tulikuwa Wakristo, kwa kuwa tulichukua au kupokea mafundisho ya upande mmoja tu. Hivi sasa sisi sio Wakristo tena, sisi ni Waislam. Hapa tulipo fikia inatosha kuufunga mjadala wetu, isipokuwa tuongeze bidii ya kujisomea zaidi juu ya dini zetu kuweza kupambanua zaidi. Kwa sasa nitawaombeni tuwe na kikao siku moja moja kwa ajili ya kutupa mawaidha tu. Nadhani hata wenzangu watakubaliana na mimi."
Sura ya "14"
Baada ya kukaa siku kdhaa, siku moja badabaada ya chakula cha jioni, walijumuika. Safari haikuwa tena ni majadiliano bali ni mawaidha yaliyotolewa y na Bwana Adul. Aliananza kwa kusema:-
"Leo tuangalie utabiri wa Mtume Muhammad ndani ya Biblia. Tukianza na na Yeremiah 28:9 inayo sema, Nabii atabiriwaye habari za amani, neno la Nabii yule litakapotokea ndipo Nabii yule atakapo julikana kuwa Bwana amemtuma kweli kweli."
"Hapa ina maana, Yeremiah kataja amani, lenye maana islamu kwa lugha ya Kiarabu. Hivyo basi Islamu maana yake ni utulivu, Amani kati ya muumba na viumbe vyake."
"Utabiri huu wa Yeremiah siyo kwa Yesu, amesema katika Luka 12:51-53 kwamba: Je, mnadadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia la, sivyo, bali mafarakano. Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwemo watu watano wamefarakana, Watafarakana watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. Watafarakana baba na mwanae, mwana babaye, mama na binti yake, na binti na mamaye, mkwe mtu na mkwe, mkwe na mkwe mtu."
"Ukiangalia Mathayo 10:34-36 inasema, Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu, na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake."
"Hivyo basi, Yeremiah anatujulisha kuwa neno la Nabii yule litakapotokea mwenye habari za amani ndipo Nabii yule atakapojulikana kuwa Bwana amemtuma kweli kweli, naye siyo Yesu bali ni Mtume Muhammad (s..w.)."
Adul aliwaambia kuwa yamkini hapo sasa wamepaelewa. Kwa tabasamu lililo kuwepo kwa kila mmoja, sauti ambazo hazikuwa na mikwaruzo zilisikika masikioni barabara na wakiitikia miitiko tofauti kuwa pameeleweka-sawa kabisa.
Adul hakuishia hapo, aliendelea kuwaambia kuwa, sasa waangalie eneo jingine, wamuone Yakobo katika Mwanzo 49:1:-
"Mwanzo 49:1 inasema, Yakobo akawaita wanae akasema, kusanyikeni, ili niwaambie yatakayo wapata siku za mwisho."
"Hapa Yakobo anakusudia kuwaambia nini wanae? Tusome Mwanzo 49:10 isemayo, Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda wala mfanya sharia kati ya miguu yake. Hata atakapo kuja yeye, mwenye miliki, ambaye mataifa watamtii."
"Yakobo aliwakusanya wanae na kuwaambia habari za Unabii utakao fuata baadaye baada ya kuondoka katika Yuda. Sio Unabii wa Yesu bali ni Mtume Muhammad (s.a.w.).
" Hivyo, Unabii kutoka uzao wa Isaka utasita mara moja ajapo Shiloh tu."
Adul aliwaomba wamvumilie ili awape kipengere kingine ili wakapumzike. Aliwarudisha nyuma kidogo akasema:-
"Neno Shiloh lina maana ya amani, salama, na utulivu yaani Islamu. Kama litatamkwa 'Shaluah Elohim maana yake ni mjumbe wa Mungu."
"Qur'an sura ya 3:13 inasema, Je, nyinyi Mayahudi na Wakristo mlikuwepo yalipomfika Yaakubu yaani Yakobo mauti, alipo waambia wanae. Je, mtamwabudu nani baada yangu? Wakasema, tutamwabudu Mola wako na Mola wa baba zako, Ibrahim na Ismaili na Is-haka; Mungu mmoja tu, na sisi tutanyenyekea kwake."
"Wanae Ibrahimu walimjibu baba yao kuwa watanyenyekea kwake Mungu mmoja tu. Ikiwa na maana watafuata Uislamu yaani Unyenyekevu."
Adul aliwatazama kila mmoja kuhakikisha kama wapo macho wote, kwani muda ulikuwa umelejea wa kulala. Aliwaomba wamalizie na na Yeremiah 31:36 na Mathayo 21:43:-
"Yeremiah 31:36 inasema, Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele yangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele."
"Mathayo 21:43 inasema, Kwa sababu hiyo nawaambia, ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu nao watapewa Taifa jingine lenye kuzaa matunda yake."
"Hizi zote ni tabiri za Unabii wa Israeli ambao ni Yesu utaondolewa na kupewa taifa jingine lenye kuzaa matunda yake, na Israeli wataacha kuwa taifa mbele ya Mola milele, ikiwa na maana ya Unabii."
Sura ya "15"
Baada ya siku kadhaa kupita, ilikuwa siku ya Ijumaa, baada ya ibada ya Ijumaa, siku hiyo, walikuwa wamempumzika nje, chini ya kivuli cha mkwaju. Ustadhi alianza kueleza kuwa:-
"Tumeliona neno Bakka ndani ya Biblia. Bakka ndiyo Makka ambako Nabii Ibrahimu na mwanae Ishmaeli walijenga nyumba takatifu yaani Ka' aba."
"Neno la asili Kiyunani ni Shilo, na kwa sababu wazielewazo wafasiri wa Biblia, walimtafasiri 'yeye'.
" Watafasiri wa Biblia ya Kiswahili Union Version ya 1952 kwa sababu zao wamelitafasiri neno Bakka ni VILIO, lakini tafasiri ya Kiingereza limebaki kama lilivyo."
"Qur'an sura ya 3:96 inatuambia: Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu kufanya ibada ni ile iliyoko Bakka yaani Makka, yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote."
"Nabii Daudi katika Zaburi 84:6 inasema, Wakipita chini ya bonde la Bakka."
Ustadhi aliondoka kwa muda, alienda kutabaruku, akawacha wanachezesha vichwa vyao huku wakitafakari yale wanayo yapata. Aliporudi aliendelea kuwambia kuwa, sasa inabidi waangalie nyumba ya utukufu katika Isaya 60:-
Isaya 60: inasema: Ondoka uangaze ; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia."
"Vile vile Qur:an 74:1-3 inasema hivi, Ewe uliyejifunika maguo simama uonye viumbe, na Mola wako umtukuze."
"Isaya 60:2 insema, Maana tazama, giza litafunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu bali Bwana atakuzukia wewe na utukufu wako utaonekana juu yako."
"Mtume Muhammad (s.a.w) alikuja wakati wa giza, watu wamesahau upweke wa Mwenyezi Mungu kama alivyofundisha Nabii Ibrahimu na Mitume wengine na Yesu."
Isaya 60:3 inasema, Na mataifa wataijilia nuru yako na wafalme kuujua mwanga wa kuzuka kwako."
"Isaya 60:4 inasema hivi, Inua macho yako, utazame pande zote, wote wanakusanyana, wanakuijia wewe. Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani."
Adul aliwaambia wapwa zake kuwa, waangalie utabiri huo , miaka isiyo pungua ishirini na tatu Bara la Arabu lote liliungana. aliendelea na maandiko:-
"Isaya 60:5 inasema hivi, , Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukuijia. Utajiri wa mataifa utakuwasilia."
Ustadhi kwa mara nyingine tena aliwafafanulia kuwa, utabiri ule uliwaonesha jinsi Uislamu ulivyo enea katika muda usiozidi karne moja katika nchi nyingi nje na bara la Arabu. Alizidi kuwaeleza kuwa:-
"Isaya 60:6 nayo inasema kuwa, Wingi wa Ngamia utakufunika, ngamia vijana wa Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Sheba; wataleta dhahabu na uvumba; na kuzitangaza sifa za Bwana."
"Isaya 60:7 inasema , Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo wa Bebayothi watakutumikia, watapanda juu ya madhahabu yangu kwa kibali, nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu."
Ufafanuzi uliendelea kutolewa tena na Ustadhi aliwaambia, ina maana kwamba, nyumba ya utukufu ni nyumba ya Mwenyezi Mungu iliyoko Makka yaani Al ka-bah wala siyo Kanisa la Yesu. Na vijiji vya Kedari kwa sasa karibu vyote ni Saud Arabia. Pia ni nchi peke yake duniani ambayo haijawa na athari ya makanisa. Sura ya Isaya ilikuwa inendelea:-
"Isaya 60:11 inanena hivi, Malango nayo yatakuwa wazi daima, hayatafungwa mchana wala usiku, ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao."
Bado ufafanuzi uliendelea kutolewa na Ustadhi. Aliwaeleza ni nini kinazungumzwa, na siyo kingine bali Msikiti unao uzunguka Ka-abah tukufu huko Makka, huwa wazi usiku na mchana tangu ulipo takaswa na Mtume Muhammad (s.a.w.) kwa masanamu miaka.1400 iliyopita. Ambako viongozi na raia wao wote huwa wanaenda kuhiji.
Aliwauliza iwapo wameelewa vizuri, kama yupo amabaye hakuelewa basi ruhusa kuuliza. Lakini hakuna aliye kuwa tayari Swali. Ndipo Ustadhi akawaomba waendelee na kuwajadili wapanda Punda na Ngamia. Je, hao ni nani? Aliwataka wasome Isaya 21:7.
"Isaya 21:7 inasema hivi, Naye akiona kundi la wapanda farasi wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia, asikilize sana, akijitahidi kusikiliza."
Ustadhi aliwaambia wapwaye, kwamba sasa wajiulize wao wenyewe, nani alikuwa mpanda punda? Aliwataka wasome Yohana 12:14:-
"Yohana 12:14 inasema hivi, Naye Yesu alikuwa amepanda mwana wa punda, akampanda kama vile ilivyoandikwa."
Wameisha ona Yesu alipanda mwana wa punda. Sasa Ustadhi aliwaambia, sasa wamtafute nani aliye kuwa mpanda ngamia? Isaya 21:13 waisome:-
"Isaya 21:13 inasema hivi, Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya mwitu wa Arabuni mtalala, enyi misafara ya Wadedani."
Hapa ina maana kuwa ufunuo uliteremshwa Arabuni kwa Mtume Muhammad ((s.a.w) na huyo ndiye aliye mpanda ngamia, Ustadhi alihoji kuwa, inakuwaje wasomaji wa Biblia wanamsahau? Waliendelea na Isaya 21:14:-
"Isaya 21:14 inasema hivi, Waleteni wenye kiu na maji, enyi wenyeji wa nchi ya Tema, nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao."
Ustadhi aliwajuza kuwa, Tema ulikuwa ni mji wa Madina ambako Mtume Muhammad ,s.a.w.) na masahaba wake walihamia, na kila sahaba alishika urafiki na mwenyeji mmoja wa Madina, wakapata chakula na nyumba za kuishi.
Aliedelea kuwafahamisha kuwa Isaya 21:15 inaweka msisitizo habari ya Mtume Muhammad (s.a.w.) na wafuasi wake walipoteswa, wakahama Makka kwenda Madina. Aya hiyo waliisoma:-
"Isaya 21:15 inasema, Kwa maana wanakimbia mbele ya upanga, upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa, na mbele ya ukali wa vita."
"Isaya 21:16 nayo inanena, Kwa sababu Bwana amwambia, hivi, katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wa Kedari."
Ustadhi aliendendelea na ufafanuzi kwamba, katika mwaka uliofuata wa Hijrah tangu Waislam walipohamia Madina makafiri walishindwa katika vita vya Badri. Aliendelea na Isaya 21:17 kwamba waisome pia:-
"Isaya 21:17 inasema, Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache, maana Bwana, Mungu wa Israel, amenena hili."
Bila ubishi, Ustadhi aliwaambia kuwa, Kedari mtoto wa pili wa Ishmaeli ambaye Mtume Muhammad ni wa nasaba yake. Hapo mwanzo Mtume Muhammad (s.a.w.) alikuwa anahujumiwa na watoto wa Kedari. Lakini kwa kuwa wengi waowaliukubali Uislamu. Watoto wa Kedari walioupinga Uislamu walipungua sana. Hivyo basi Kedari imetumika kwa maana ya Arabuni kama ilivyo katika Ezekiel 27:21 iliyo nena kuwa:-
"Ezekiel 27:21 inasema, Arabuni na wakuu wote wa Kedari."
Mwanzo 25:13, Ustadhi alisisitiza kwamba, aya hiyo inathibitisha kwamba Kedari ni mtoto wa pili wa wa Ishmael, alinukuu:-
"Mwanzo 25:13 inasema hivi Na haya ndiyo majina ya wana Ishmaeli, kwa majina yao na vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu.
Sura ya "16"
Waliendelea na mazungumzo yao kama kawaida. Hii ilikuwa ni siku iliyo fuata. Safari hii mjoba wao Ustadhi aliwapeleka kuangalia habari ya ya Nabii Musa Mwenyezi Mungu alipo mwambia katika Kumbukumbu: 28:28, waliisoma wote kwa pamoja:-
"Kumbukumbu 18:18 inasema kuwa, Mimi nitawaodokeshea Nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayo mwamuru."
Usitadhi alianza kufafanua kuwa, kwanza kabisa, ndugu wa Wayahudi ni uzao wa Nabii Ibrahimu kupitia Isaka. Ndugu wa Mwarabu ni uzao wa wa Ibrahimu kupitia Ishimaeli. Kwa vyovyote Yesu alikuwa Myahudi, kipengere hiki hakimhusu kabisa. Vinginevyo ingesema: Nabii kutoka miongoni mwenu.
Jambo la pili, Mtume Muhammad ni mfano wa Musa. Jarida la Al-Ittihad la Januari-Machi 1982 ukurasa wa 41 limetoa mlinganisho wa baadhi ya sifa muhimu za Nabii Musa, Muhammad na Isa 'amani iwe juu yao wote' ambazo zinabainisha ni nani hasa 'Nabii yule' aliyekuwa anatarajiwa baada ya Mussa. Ustadhi aliwaambia sasa waangalie sifa zao, ya kwanza:-
"Sifa ya kwanza: Kuzaliwa kwa kawaida. Musa, Muhammad walizaliwa kwa njia ya kawaida, isipokuwa Yesu alizaliwa kwa miujiza.
"Sifa ya pili: Kuwa na familia. Musa na Muhammad walioa na walizaa. Yesu hakuoa wala kuzaa.
"Sifa ya tatu: Kifo. Musa na Muhammad walikufa kifo cha kawaida. Yesu sio cha kawaida.
" Sifa ya Nne: Cheo. Musa na Muhammad walikuwa Mitume na Watawala. Yesu alikuwa Mtume."
"Sifa ya tano: Ulazimisho. Musa na Muhammad walilazimishwa kuhamia Madina. Yesu hakulazimishwa popote."
"Sifa ya Sita: Kupigana Vita. Musa na Muhammad waliandamwa na kupigana. Yesu hakupigana.
"Sifa ya Saba: Ushindi. Musa, Muhammad na Yesu, walishinda vita vya dini.
"Sifa ya Nane: Wahyi. Katika uhai wao. Musa alikuwa na Taurati, Muhamamad alikuwa na Qor'an na Yesu ilikuwa ni Ijili baada ya kuondoka kwake.
"Sifa ya Tisa: Mafundisho. Musa na Muhammad walifundisha dini na sheria. Yesu alifundisha dini.
"Sifa ya ya Kumi: Uongozi. Musa na Muhammad walikataliwa kuwa viongozi kisha wakakubaliwa. Yesu alikataliwa na wengi wa Israel."
Ustadhi aliendekea na ufafanuzi kwamba, Wahyi wa Mwenyezi Mungu ni kama vile neno lisemalo, "Nitatia maneno yangu kinywani mwake". Huo ulikuja kupitia Malaika Jibril (a.s.) na wala hazikuwa fikra na Muhammad (s.a.w.) binafsi. Ndivyo ilivyo kwa Wahyi wowote ulio teremshwa na Mwenyezi Mungu (s.w.). Huenda kutajwa huko ni makusudi, ikilinganishwa na Wahyi aliotelemshiwa Nabii Musa katika mbao zilizo andikwa kama inavyoaminiwa.
Alizidi kuwapa elimu kuwa, ndiyo maana katika Qur'an yenye sura mia moja na kumi na nne. Sura mia moja na kumi tatu zimeanza na jina la :
"Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu."
Pia katika kufanya kila kitu, kawaida huanza kwa maneno hayo. Hivyo basi jina la ALLAH haliwezi kubadirishwa kama ilivyo kiingereza Mungu au Mungu mke yaani God or Godess au katika wingi God or Gods. Kwa wenzetu Wakristo huanza na :-
"Kwa jina la Baba, mwana na Roho mtakatifu."
Ustadhi alizidi kuwaambia wasome Kumbukumbu 18:19 na kisha aliifafanua ikiwa na maana kuwa, wasio msikiliza yeye, au watakao mpinga, wataadhibiwa. Hii ni sa wa na Qur'an Tukufu sura 3:19. Nayo sura ya 3:85 inasema:-
"Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi hatakubaliwa kwake. Na akhera atakuwa mwenye kula hasara kubwa kabisa."
Ustadhi aliwataka wapwaye wapumzike hadi hapo watakapo jaliwa na Mwenyezi Mungu, ili wakutane tena waweze kuumalizia mjadala wao.
Baada ya mapumziko ya siku mbili tatu, walikutana tena. Awamu hii waliegemea katika maneno ya 'Mtumishi', 'Mjumbe', 'Mteule' yalivyo tumika. Walianzia na Isaya 42:1 na 42:19:-
"Isaya 42:1 inasema hivi, tazama Mtumishi wangu nimtegemeaye, Mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimemtia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu."
"Isaya 42:19 inasema kuwa, Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu, kama mtumishi wa Bwana?
Ustadhi aliendelea kuwafahamisha kuwa, aya zote mbili zimetumia maneno yale yale, hivyo basi bila shaka yoyote ni kwamba Mitume wote walikuwa ni watumishi, Wajumbe na Wateule wa Mwenyezi Mungu (s.w.). Hata hivyo ni Mtume Muhammad (s.a.w.) peke yake ndiye aliyeitwa kwa maneno hayo kama ilivyo katika Kiarabu:-
"Abduhu wa Rasuluhul Mustafa." maana yake ni (Mtumishi, na Mjumbe wake Mteule.)"
Alizidi kuwaeleza kuwa, pia mtu anaposilimu hutoa shahada kwa kutamka:-
"Nashuhudia kwamba, hapana Mungu, isipokuwa Allah peke yake asiye na mshirika, na nakubali kuwa Muhammad ni Mtumishi na Mjumbe wake."
Ustadhi aliendelea kufafanua kuwa, maneno hayo hurudiwa mara tano kwa siku itolewapo Adhana yaani wito wa Sala. Pia hutamkwa mara tano kabla ya kila sala yaani Iqama.
Vile vile maneno hayo hurudiwa mara tisa katika sala za wajibu. Tashhud. Na hata katika sala za sunna hutajwa maneno hayo mara chungu nzima.
Hivyo basi jina au sifa maarufu iliyotumika kwa Mtume Muhammad ni:-
"Rasulullah" (yaani mjumbe wa Mwenyezi Mungu)."
Ustadhi aliendelea kuwa, katika Isaya 42:2 aya hii inaonesha heshima na adabu aliyokuwa nayo Muhammad (s.a.w.) kwani ilisomeka hivi:-
"Hatalia wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu."
Aliwaomba wapwa zake waendelee kuisoma Isaya 42:4 hadi 42:13:-
"Isaya 42:4. Inasema, Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapo weka hukumu duniani, na visiwa vitaingojea sheria yake"
Ustadhi alifafanua kuwa, wao husema kwamba aya hii ni Yesu. Lakini kama Yesu, mbona hakuweza kuwashinda maadui zake, na alichukizwa sana alipo kataliwa na Mayahudi? Aliwaambia waendelee na Isaya inayofuata:-
"Isaya 42:6 inasema, Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa. Na nakulinda."
Aya hii ina maana, hakuna Mtume mwingine atakaye kuja baada yake. Zaidi alifafanua na kuendelea kuwa: Watu wa mataifa, wengi waliukubali Uislamu. Aliwaambia waendelee na aya inayofuata:-
"Isaya 42:7 inasema kuwa, Kuyafufua macho ya upofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walio keti gizani katika nyumba ya kufungwa."
Hii ina maana kuwa, macho ya upofu walio keti gizani ni maisha ya kipagani; na kuwatoa gerezani walio fungwa, inaashiria ni kuondoka kwa watumwa mara ya kwanza katika historia ya uwanadamu. Ustadhi aliwaeleza na alisisitiza aya ifuatayo isomwe na Zainab (Love):-
"Isaya 42:8 inanena hivi, Mimi ni Bwana, ndiyo jina langi, utukufu wangu nitampa mtu mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu."
Usitadhi alisema, aya inamaanisha kuwa , yeye ni Mungu pekee, hatampa mtu mwingine baada Mtume Muhammad (s.a.w.) kwa kuwa ndiye mwisho wa Manabii, na mafundisho yake bado hayajachafuliwa hadi sasa ukilinganisha na Ukristo.
"Isaya 42:10 nayo inasema, Mwimbieni Bwana wimbo mpya, na sifa zake tokea mwisho wa dunia."
Ustadhi aliwafahamisha kuwa, wimbo huo haupo katika Kiabramu wala Kiaramu bali ni kwa Kiarabu na maana yake ni sifa za Mwenyezi Mungu na mtume. Husein aliendelea na aya nyingine:-
"Isaya 42:11: inasema, Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, vijiji vinavyo kaliwa na Kedari, na waimbe Wenyeji wa Sela, wapige kelele toka vilelele vya milima."
Aya hii inaashiria kuwa, vilima vya arafat karibu na mji wa Makka wahujaji husema kwa pamoja kwa sauti ya juu maneno yafuayao:-
"Nimeitika wito wa kukutumia wewe ewe Mola, nimeitikia. Nimeitikia huna mshirika, nimeitika. Sifa zote njema utukufu , ufalme ni wako wewe tu huna mshirika."
Hivyo basi, Ustashi alisema kuwa, ndiyo kusema aya hii Isaya 42 haimuhusu . Mtume wa Kiisraeli kwani Kedari ni mtoto wa pili wa Ishmaeli, kama tulivyoona huko nyuma katika Mwanzo 25:13. Waliendelea na aya iliyofuatia:-
"Isaya 42:12 inasema hivi, Na wamtukuze, kutangaza sifa zake visiwani."
Hapa bila ubishi ina maana ya kuwa, Uislamu umeenea katika visiwa vidogo vidogo vya Indonesia na bahari ya Caribean.
"Isaya 42:13 inasema kwamba, Atawatenda adui zake mambo Makuu.."
Aya hii inamaanisha kuwa, ilichukua muda mfupi ambapo ufalme wa Mwenyezi Mungu ulionekana kwa ujio wa Mtume Muhammad (s.a.w.).Hivyo Sura hii ya Isaya , sifa zote zilizomo ni Mtume Muhammad (s.a.w.).
Ustadhi alimaliza, aliwaacha wenzake wana nong'ona hili na lile ndipo aliposema kuwa sasa waone neno 'Bwana' lina maana gani ambalo limetajwa kwenye Zaburi 110:1.,
Sura ya "17"
Kikao chao kilianza na mjadala wa neno 'Bwana' kwamba lina maana gani? Neno hilo ambalo limetumika katika Zaburi 110:1, ambayo Abubakar (Kibon) aliisoma mbele yao:-
Zaburi 110:1. Inasema hivi, Neno la Bwana kwa Bwana wangu, uketi mkono wa kuume, hata niwafanyapo adui zako kuwa chini ja miguu yako."
Hapa Ustadhi aliwaambia wenzake kwamba, katika aya hiyo wametajwa mabwana wawili. Kuna msemaji na na mwenye kuambiawa. Je, nani kati ya hao ni Mungu? Lakini Kanisa linasena huyo ni Yesu. Pia Daudi anamfahamu Mungu ni mmoja tu. Yesu mwenyewe alikataa katika Mathayo 22:45 isemayo:-
"Basi Daudi akamwita Bwana, imekuwaje ni mwanae?" Mathayo 22:45.
Maneno ya kwenye aya hiyo yamejirudia katika Marko 12:37. Ismail aliendelea kuwapa darasa kwamba, isitoshe Yesu alijivua sifa hiyo kwani alijua kabisa kwamba yeye ni mtoto wa Daudi na akasema katika Luka 20:41-44
"Luka 20:41-44 ina nena, Akamwambia, wasemaje watu kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?"
Hivyo basi Ustadhi alendelea kuwaeleza kwamba, kwa vyovyote Yesu alitoa jibu, ambalo halikuandikwa kwenye vitabu vyote vinne vya Injili, lakini limetajwa waziwazi kwenye injili ya Barnaba kwamba Agano lilifanywa na Ishmaeli na siyo Isaka. Hivyo Bwana wa Daudi alikuwa Mtume Muhammad (s.a.w.) ambaye alimuona Roho. Muhammad ni Mtume pekee aliye fanikiwa zaidi kwa muda mfupi wa uhai wake. Mafanikio yake yalibaki bila mabaliko hadi leo.
Baada ya mjadala wa neno hilo kumalizika. Waliingia kwenye mjadala wa neno jingine amabalo ni 'Wewe U Nabii yule?' Abubakari aliendelea kuwasomea aya hiyo:-
"Yohana 1:20-21 inasema hivi, Naye alikiri, wala hakukana, alikiri mimi siye Kristo. Wamuuliza Ni nani basi? U Eliya wewe? Akasema mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu la."
Ustadhi aliendelea na ufafanuzi wake kwamba, aliyekuwa anasubiriwa baada ya Yesu na Yohana Mbatizaji, kwa muda mrefu alikuwa ni Mtume Muhammad (s.a.w.) ambaye ni mfano wa Musa kama ilivyo kwenye Kumbukumbu 17:18
Mjadala huo nao ulikuwa kama umeisha, lakini pakazuka jambo jingine la 'Kubatiza kwa Roho Mtakatifu naMathay kama ilivyo katika Mathayo 3:11 naye (Husein (Kahin) aliwasomea :-
"Mathayo 3:11 inasema, Kwani mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili toba, bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sisitahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto."
Maneno haya ni ya Yohana Mbatizaji. Ustadhi alizidi kufafanua. Ingelikuwa aliyekusudiwa ni Yesu, Yohana Mbatizaji asinge rudi kuishi nyikani, bali angelikaa naye akawa mmoja wapo wa wanafunzi wake. Nabii mwingine mwenye nguvu aliyekusudiwa siyo Kristo, kwani ajaye baada ya Yohana Mbatizaji hawezi kuwa Yesu. Kwa sababu wote wawili kwa wakati mmoja walikuwepo. Yohana mwenyewe amesema "ajae baada yake ". Je, hapa hapo si Mtume Mtume Muhammad (s.a.w) aliyekusudiwa na Yohana Mbatizaji?
Bado kulikuwa na jingine ambalo lilinukuliwa katika Mathayo 11:11. Adul aliwasomea:-
Mathayo 11:11 inasema, Amin, nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbiguni ni mkuu kuliko yeye."
Swali lilikuwa, ni nani aliye mdogo katoka ufalme wa mbiguni?. Ismail alisema kuwa, ukweli siyo Yesu, kwani kipindi hicho ufalme wa mbiguni ulikuwa haupo, Yesu mwenyewe hakudai udogo. Ufalme wa mbinguni ni wake Mwenyezi Mungu na Mitume wote. Mdogo kwa mjibu wa aya hii ni Mtume Muhammad (s.a.w.).
Hapo hapo lilifuatia neno jingine amabalo linapatikana katika Mathayo 6:9 lisemalo:-
"Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu."
Hapa ina maana kwamba, isimail aliwaambia, neno mpatamnishi lina maana kuleta amani, ama Islam kwa kiarabu. Yesu hakuwa mpatanishi kwani hakuja kuleta amani kama Mathayo inavyosema:-
"Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nilikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu. Mathayo 10:34-36 na Luka 12:49-63."
Hivyo basi kwa mujibu wa aya hiyo, Yesu ni dhahiri hakuleta amani duniani, bali ni Mtume Muhammad (s.a.w.)
Sura ya "18"
Baada ya siku kadhaa kupita kupita walikaa tena kuendendelea na mazungumzo yao ambayo walidai kuwa utakuwa ni mjadala wa mwisho, ingawa utakuwa ni mrefupi.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya mwisho wa juma. Mjadala wao kuwa ni neo "Msaidizi." ambalo linapatikana kàtika Yohana 14:16 linalo someka kama alivyowasomea Husein (Kahin):-
"Inasema hivi Yohana 14:16, Mimi nitamuomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele."
Pamekuwa na utata. Ismail alisema, utata huo ni neno gani Kiaramu alilolitumia Yesu badala ya msaidizi, wengine husema ni Mfariji au Muombezi katika Biblia kadhaa.
Aliwapeleka kwenye Qur'an Tukufu sura 61:6 inasomeka kama alivyo wasomea Abubakari (Kibon) :-
"Na wakumbushe waliposema Nabii Isa bin Mariam kuwaambia Mayahudi: Enyi wana wa Israeli, mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu yangu katika Taurati, na kutoa habari njema ya Mtume atakaye kuja baada yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad jina la pili la Mtume Muhammad, na lina maana ya mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu zaidi kuliko wengine."
Kwa maelezo hayo ya Biblia na Qur'an, inakubalika kuwa Yesu aliondoka na hakumaliza kazi, na ndiyo maana ikabidi Msaidizi aje kuikamilisha sehemu aliyoiacha.
Ustadhi aliwaambia wapwa zake kuwa, sasa inabidi waangalie kwa undani zaidi katika Biblia kama huyo Msaidizi analingana na sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.).
Kwanza Ustadhi alianza na "Msaidizizi Mwingine" Wasaidizi wengi walikuja kabla na mwingine alikuwa aje.
Pili, "Ili akae nanyi milele." Hakutarajiwa mwingine baada ya huyo ajae, ilikuwa ndiyo mwisho wa Mitume. Mafundisho yake yatabaki milele pasipo kuchafuliwa. Iliyobaki ni Qur,an kama ilivyo teremshwa miaka chungu nzima iliyopita.
Tatu,"Atauhakikisha-atakataza" ulimwengu kwa habari ya dhambi. Yohana.16:18.
Nabii Ibrahim, Musa, Daudi na Suleiman waliwaadhibu majirani zao na watu wao kwa sababu ya dhambi. Lakini hawakufanya hivyo kwa ulimwengu mzima. Mtume Muhammad hakuondoa masanamu tu bali pia wajumbe wa Heraclius na kwa wafalme wa madola ya Fursi na Roma, kwa Najashi mfalme wa Ethopia vilevile kwa Mugangis Gavana wa Misri.
Mtume Muhammad (s.a.w.) ndiye aliye washutumu Mayahudi na Wakristo kwa kuviharibu vitabu vya Mwenyezi Mungu, alionesha uhalali wa kuzaliwa Nabii Ishmaeli (a.s.) na akasafisha heshima zao dhidi ya tuhuma za uzinifu, kufanya mambo machafu na watoto wao, kuwanajisi wanawake kwa nguvu na kukomesha ibada za masanamu.
Nne, "Yule Mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumu. Yohana 6:11. Huyu ni shetani imeelezwa katika Yohana 12:31 na 14:39. Mtume Muhammad amekuja kuhukumu ulimwengu.
Tano, Huyo Roho wa kweli Yohana 16:13. Mtume Muhammad (s.a.w) tangu utotot wake aliitwa Al - Amin, yaani Mwaminifu au Mkweli, na atawaongoza awatie kweli yote."
Sita, Kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atayasikia atayanena. Yohana 16:13.
Malaika Jibril alikuwa akimsomea Mtume Muhammad (s.a.w.) Qur'an, naye aliihifadhi pia kuandikwa na wandishi wake. Mafundisho na maneno yake Mtume Muhammad (s.a.w.) yameandikwa katika hadithi na wala sio ndani ya Qur'ana. Tukufu ni nejo la Mwenyezi Mungu.
Saba, "Na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yohana 16:13."
Mtume Muhammad (s.a.w.) aliyo yatabiri yalitokea kama alivyo tabiri.
Nane, "Yeye atanitukuza mimi". Yohana 16:14.
Ukweli ni kwamba Qur'an, na Mtume Muhammad (s.a.w) ni heshima kubwa zaidi kwa Yesu (a.s.) kuliko jinsi inavyo mheshimu Biblia na Wakristo wenyewe, nikiwa na maana kuwa:
Mosi, Kuamini kuwa Yesu alikufa msalabani ni kuutweza utume wake. Kwani Kumb:13'5 inasema:-
"Na yule nabii, au yule muota ndoto, na auawe."
Pia kumb: 21:22-23 inasema:
"Kwani aliye tundikwa amelaaniwa na Mungu.
Pili, "Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?"
Hii ni kebehi kwa Yesu kwamba alikuwa hana imani juu ya Mwenyezi Mungu. Maneno hayo yalitoka kinywani mwa Yesu, hivyo hata asiye nabii angefurahia mateso kwa kujua kuwa kifo chake kitampa cheo cha ushuhuda.
Tatu, Waislamu hatuamini kuwa Yesu alisema katika Mathayo 7:6:-
"Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya Nguruwe."
Pia Yohana 2:4 inasema:-
"Yesu akamwambia, tuna nini mimi nawe?"
Qur'an sura ya 19:32 imetiambia kuwa:-
"Na Mwenyezi Mungu amenihusia kumfanyia mema mama yangu, wala hamkunifanya niwe jeuri, muovu."
Kwa kumalizia, ufunuo ama wahyi wa kwanza wa Mtume Muhammad (s.a.w.) ilikuwa ni neno "Iqraa" mana yake "soma".Qur'an 96:1-5.
"Kwa kuwa alikuwa hajui kisoma wala kuandika alijibu 'siwezi kusoma'."
Pia imetabiriwa katika Isaya 29:12
"Chuo hiki apewa mtu asiye maarifa , akaambiwa akisoma hicho tafadhali, 'sina maarifa mimi'.
Ufunuo au wahyi wa Qur'an uliteremshwa kidogo kidogo , na kwanza haupo ukurasa wa kwanza na mwisho. Kama zilivyo mipangilio mingine. Hivyo katika miaka 23 wahyi uliwekwa kwa mpango maalum ulioelekezwa na Mwenyezi Mungu (s.w.) kama ilivyo katika Isaya 28:10-11:-
"Kwa maana ni amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo, na huku kidogo. La bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa."
Lugha iliyo zungumzwa ni kiarabu, Waisalamu duniani kote wanatumia lugha moja tu ya Kiarabu katika katika ibada zote na hata hata kuamkiana kama inavyosema Zefania 3:9.
"Maana hapo ndipo nitakapo warudisha mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliita jina la Bwana, wamtumikie kwa kwa mia moja."
Bado wengine wanamtarajia Yesu kwa mujibu wa maelezo hayo. Sisi Waislamu tunaamini, Yesu atakuja kwa mara ya pili, ataungana na Waislamu msikitini wakiwa na tohara, hatakula nguruwe,
atasali akiwa na udhu, kwa kusimama, kurukuu na kusujudu.
Sura ya "19"
Wakati wote wa mazungumzo yao, mzee Busa alikuwepo lakini hakuwahi kutia neno. Yeye alikuwa msikilizaji tu. Lakini kwa upande mwingine alikuwa na furaha kumuona mwanae aliye kuwa ametoweka kwa miaka mingi amerudi, amerudi akiwa na watoto yaani wajukuu zake.
Ingawa kulikuwa na changamoto kadhaa zilizo wahi kumtokea huyo binti yake. Mzee Busa alikuwa na yake moyoni, kwanza kabisa alimwita binti yake Tamaa (Amina). Binti alipiga magoti mbele ya baba yake, alimwekea mkono juu ya kichwa chake kisha alitoa kauli ya:-
"Mwanangu, iwapo tuliwahi kufanyiniana makosa, leo iwe ni siku ya kusameheana."
"Pili, kurudi kwako, ukiwa na wajukuu zangu ni faraja kwangu pia ni mipango ya Allah."
"Tatu, sahau changamoto ulizozipitia. Chagua eneo lolote litakalo kufaa ufanye maenndeleo yako ya maisha."
"Nne, fungamana na nduguzo kudumisha upendo nyiyi na uzao wenu."
"Tano, kuanzia sasa atakuwepo shekh atakaye kuwa anatoa mafundisho ya imani yetu ya Kiislam, na hasa kwa hawa wajukuu zangu."
"Sita, sisi sote hapa imani yetu ni moja. Mimi mwenewe jina langu halisi ni RAMADHANI. Mke wangu ni ZILIFA. Mjomba wenu huyu mnawita Ustadhi, jina lake ni ISMAIL. Huyu Adul ni ABDUL, mama yenu mdogo Kulut jina lake halisi ni KULTHUMU.
Mwisho kabisa naufunga mjadala huu kwa kusema, Mwenyezi Mungu atuwezeshe kwa kila lililo jema na kheri. Inshallah.
Wote waliitikia " INSHALLAH-INSHALLAH-INSHALLAH"
No comments:
Post a Comment